Kushiriki video za YouTube
-
Anza kutazama video kwenye youtube.com.
-
Chini ya sehemu ya video, bofya Shiriki .
- Kidirisha kitafunguka, kikionyesha chaguo tofauti za kutuma:
- Mitandao ya kijamii: Bofya aikoni ya mtandao husika wa kijamii (kwa mfano, Facebook au X) ili utume video huko.
- Barua pepe: Chagua aikoni ya barua pepe ili utume barua pepe ukitumia programu chaguomsingi ya barua pepe kwenye kompyuta yako.
- Kupachika Bofya kitufe cha Pachika ili utunge msimbo unaoweza kutumia kupachika video katika tovuti.
- Kunakili kiungo: Bofya kitufe cha Nakili ili unakili kiungo cha video ambacho unaweza kubandika kwingineko, kama vile katika ujumbe wa barua pepe.
- Anzia: Ili upate kiungo kinachoelekeza kwenye sehemu mahususi ya video, teua kisanduku hiki na uweke muda wa kuanzisha kabla ya kunakili kiungo. Kwa mfano, kuianzisha video katika dakika ya 2 na sekunde 30, teua kisanduku na uweke “2:30.”
- Chapisho la jumuiya: Iwapo una idhini ya kufikia kichupo cha Jumuiya, unaweza kutuma video kwenye chapisho la umma.
Kushiriki chaneli za YouTube
- Nenda kwenye Ukurasa wa chaneli.
- Katika sehemu ya anwani ya kivinjari, nakili URL.
- Bandika URL popote unapotaka kushiriki.
Iwapo ungependa kutayarisha URL maalum ya chaneli ili uitume kwa urahisi, weka jina la Chaneli yako ya YouTube kwenye URL ya YouTube.