Ukiongeza video kwenye orodha ya Tazama Baadaye, utaweza kuzipata kwa urahisi wakati wowote.
Fuatilia Chaneli ya Watazamaji wa YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.
Kuweka maudhui kwenye orodha ya kucheza ya Tazama Baadaye
- Unapotazama video: Gusa Hifadhi . Gusa BADILISHA ili ufungue orodha zako za kucheza na uchague Tazama Baadaye au orodha nyingine ya kucheza.
- Unapotazama Video fupi: Gusa Zaidi Hifadhi kwenye orodha ya kucheza Tazama Baadaye.
- Unapovinjari video: Gusa Zaidi karibu na jina la video Hifadhi kwenye Tazama Baadaye.
Ikiwa video imebainishwa kuwa inalenga watoto, huwezi kuiweka kwenye orodha ya kucheza au kuihifadhi katika orodha ya Tazama Baadaye.
Kuondoa maudhui kwenye orodha yako ya video ya Tazama Baadaye
- Gusa picha yako ya wasifu ili upate kichupo cha Wasifu.
- Chini ya “Orodha”, chagua Tazama baadaye .
- Gusa Zaidi karibu na video ambayo ungependa kuondoa.
- Gusa Ondoa kwenye orodha ya Tazama Baadaye.