Kufuta au kuficha Chaneli yako ya YouTube

Unaweza kuamua kuficha maudhui kwenye chaneli yako kwa muda au kufuta kabisa chaneli yako.

How to hide or delete your YouTube channel

Fuatilia Chaneli ya Watazamaji wa YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Kuficha chaneli yako kwa muda 

Unaweza kuficha maudhui kwenye chaneli yako ya YouTube na kuyarejesha tena baadaye. Kuficha chaneli yako kutafanya jina la chaneli, video zako, alama za kupenda, usajili na wanaofuatilia kuwa wa faragha.

Kuficha chaneli au maudhui ya chaneli yako:

  1. Ingia katika Studio ya YouTube.
  2. Kwenye utepe wa kushoto, bofya Mipangilio .
  3. Bofya Chaneli kisha Mipangilio ya Kina.
  4. Kwenye upande wa chini, bofya Futa Maudhui kwenye YouTube.
    1. Kumbuka: Kiungo hiki kitakuelekeza kwenye ukurasa ambako utaweza kufuta au kuficha chaneli yako. Huenda ukahitajika kuweka maelezo ya kuingia katika akaunti.
  5. Chagua Ningependa kuficha chaneli yangu.
  6. Teua visanduku ili uthibitishe maudhui yatakayofichwa kwenye chaneli yako.
  7. Chagua Ficha chaneli yangu.

Iwapo ungependa kufanya maudhui yako yaonekane na wengine, au ikiwa unataka kupakia video, kutoa maoni au kutumia orodha za video, unaweza kuruhusu tena chaneli iitumike.

Futa chaneli yako kabisa

Kufunga chaneli yako ya YouTube kutafuta kabisa maudhui yako, ikijumuisha video, maoni, ujumbe, orodha (za kucheza) na historia. Kumbuka kuwa, kwa sasa huwezi kufuta chaneli kwenye vifaa vya mkononi.

Ukiamua kufuta chaneli yako kabisa, huenda ikawa vigumu kurejesha akaunti yako.

Kufuta chaneli yako ya YouTube:

  1. Ingia katika Studio ya YouTube.
  2. Kwenye utepe wa kushoto, bofya Mipangilio .
  3. Bofya Chaneli kisha Mipangilio ya Kina.
  4. Kwenye upande wa chini, bofya Futa Maudhui kwenye YouTube. Ikihitajika, weka vitambulisho vyako vya kuingia katika akaunti.
  5. Chagua Ningependa kufuta maudhui yangu kabisa.
  6. Teua visanduku ili uthibitishe kuwa ungependa kufuta chaneli yako.
  7. Chagua Futa maudhui yangu.

Huenda ikachukua muda kwa chaneli yako kufutwa kabisa. Kwa muda mfupi unaweza kuendelea kutazama vijipicha vya video zako kwenye tovuti.

Kumbuka: Hatua hizi zitafuta tu chaneli yako ya YouTube, wala si Akaunti yako ya Google unayotumia kuingia. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kufuta Akaunti yako ya Google.

Baada ya kufuta chaneli, URL na jina la chaneli hazitaonekana tena wala kupatikana katika Takwimu za YouTube. Data inayohusishwa na chaneli yako, kama vile muda wa kutazama, itasalia sehemu ya ripoti za ujumlisho, lakini haitahusishwa na kituo ulichofuta.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
6823092317437863184
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true