Kudhibiti Vituo vya YouTube

Huenda ukaona mitajo mipya ya "Akaunti ya Biashara" katika chaneli yako ya YouTube au ukaona akaunti mpya katika kibadilisha akaunti chako. Hii ni kwa sababu kituo chako kiliunganishwa kwenye Akaunti ya Biashara wakati wa sasisho la hivi majuzi la YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusuchaneli zilizohamishiwa kwenye Akaunti za Biashara.

Unaweza kuweka mipangilio ya Vituo vyako vya YouTube ili uvudhibiti wewe mwenyewe tu au na watu wengi. Unaweza kuchagua kati ya chaguo zifuatazo za chaneli ya YouTube:

  • Kiunganishe kwenye Akaunti yako binafsi ya Google: Kituo kitatumia jina na picha la Akaunti yako ya Google.
  • Iunganishe kwenye Akaunti ya Biashara: Chaneli ya YouTube inaweza kutumia jina tofauti na lile unalotumia kwenye Akaunti yako ya Google.

Tunakuhimiza uunganishe kituo chako kwenye Akaunti ya Biashara au Akaunti yako binafsi ya Google. Kuunganisha kunaweza kusaidia kuthibitisha utambulisho wa kituo chako.

Tumia Akaunti yako ya Google

Akaunti ya Google ni mahususi kwa mtu mmoja tu, hivyo inatumia jina na utambulisho mmoja kwenye huduma zote za Google, ikiwa ni pamoja na kwenye chaneli yoyote ya YouTube iliyounganishwa.

unganisha akaunti ya google kwenye kituo chako cha YouTube

Ukiunganisha chaneli yako ya YouTube kwenye Akaunti yako ya Google:

  • Anayeweza kudhibiti chaneli: Ni wewe tu unayeweza kufikia chaneli ya YouTube na ni lazima utumie Akaunti yako ya Google.
  • Jina na picha ipi inayoonyeshwa: Chaneli ya YouTube hutumia jina na picha ile ile iliyoko kwenye Akaunti yako ya Google (na kwenye huduma zako nyingine za Google, kama vile Gmail au Hati za Google).

Kutumia Akaunti ya Biashara

Chaneli ya YouTube iliyounganinshwa na Akaunti ya Biashara inaweza kuruhusiwa ifikiwe kwenye akaunti nyingi.

Ukiunganisha chaneli yako ya YouTube kwenye Akaunti ya Biashara:

  • Anayeweza kudhibiti na kumiliki chaneli: Akaunti nyingi za Google zinaweza kudhibiti na kumiliki Akaunti ya Biashara na yeyote kati ya wasimamizi na wamiliki hao anaweza pia kufikia chaneli ya YouTube iliyounganishwa kwenye Akaunti ya Biashara. Ukiweka wamiliki wengine kwenye kituo, wanaweza kutekeleza vitendo kamili kwenye kituo, ikiwa ni pamoja na kufuta kituo na kuwaondoa wamiliki wengine.
  • Jina na picha inayoonyeshwa: Chaneli ya YouTube inaweza kuwa na jina na picha tofauti na Akaunti yako ya Google na Akaunti za Google za msimamizi yeyote.

Kutumia Akaunti za Biashara zinazodhibitiwa na Akaunti yako ya Google.

Unaweza kutumia Akaunti moja ya Google kudhibiti Akaunti nyingi za Biashara zilizounganishwa kwenye vituo vya YouTube.

Ukiunganisha chaneli ya YouTube kwenye Akaunti ya Biashara inayodhibitiwa na Akaunti yako ya Google pekee:

  • Nani anaweza kudhibiti kituo: Ikiwa umeunganisha vituo vingi vya YouTube kwenye Akaunti za Biashara, unaweza kuzidhibiti zote kupitia Akaunti moja ya Biashara bila kuondoka kwenye akaunti. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kubadili kati ya vituo unavyodhibiti.
  • Jina na picha inayoonyeshwa: Chaneli ya YouTube inaweza kuwa na jina na picha tofauti na Akaunti yako ya Google na Akaunti zozote za Biashara inazodhibiti.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7532294569008118568
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false