Vigezo vya muundo wa faili za sauti na video

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika wanaotumia Kidhibiti Maudhui cha YouTube kudhibiti maudhui yao yaliyo na hakimiliki.
Sharti uwe mwenye hakimiliki au mwakilishi aliyeidhinishwa wa mwenye hakimiliki kwa faili zote za video na sauti unazopakia kwenye YouTube.

Mwongozo kuhusu muundo wa video

Mwongozo ufuatao unatoa maelezo kuhusu vigezo vya muundo vinavyowezesha video zinazochezwa kwenye YouTube kuwa zenye ubora wa juu zaidi. YouTube inawahimiza washirika kupakia video ambazo muundo wao unakaribiana kabisa na muundo halisi, wenye ubora wa juu kadri iwezekanavyo ili kuongeza uwezekano wa video zako kuchezwa katika ubora wa juu zaidi (HQ). Kumbuka, YouTube husimba upya video kila wakati ili kuziboresha.

  • Muundo wa faili: YouTube inapendelea muundo halisi wa 1080p HD ulio katika maktaba yako ya maudhui ya kidijitali na mitiririko ya MPEG-2 katika muundo wa DVD iliyohifadhiwa na kiendelezi cha .MPG. Iwapo huwezi kupakia video katika muundo wa MPEG-2, chaguo mbadala linalopendelewa ni MPEG-4. Vigezo vifuatavyo vinasaidia kudumisha ubora wa juu katika uchezaji wa video za MPEG-2 na MPEG-4:

    • MPEG-2

      • Kodeki ya sauti: MPEG Layer II au Dolby AC-3
      • Kasi ya biti ya sauti: kbps 128 au zaidi
    • MPEG-4

      • Kodeki ya video: H.264
      • Kodeki ya sauti: AAC
      • Kasi ya biti ya sauti: kbps 128 au zaidi
  • Kima cha chini cha muda wa kucheza sauti na video: Sekunde 33 (bila kujumuisha picha nyeusi na tuli katika kituo cha video pamoja na kimya na kelele za mazingira katika kituo cha sauti)

  • Kasi ya picha: Kasi ya picha ya video zako inapaswa kubaki katika hali yake halisi bila kubadilisha pikseli. Kwa vyanzo vinavyotokana na filamu, video kuu yenye kasi ya 24fps au 25fps huleta matokeo bora zaidi. Kwa kawaida, kasi ya picha huwa fremu 24, 25 au 30 kwa sekunde. Tafadhali usibadilishe pikseli katika video kwa sababu hili linaweza kusababisha picha kutikisika na mara nyingi hufanya video iwe na ubora wa chini zaidi. Mifano ya mbinu isiyofaa ni pamoja na michakato ya kuongeza pikseli na kuhamisha video kama vile kwa kubadilisha kasi ya filamu ili ilingane na kasi ya video.

  • Uwiano: Unapaswa kudumisha uwiano halisi wa video. Video unazopakia hazipaswi kamwe kujumuisha upau wa mistari pana ya mlalo inayopangwa juu na chini ya picha wala mistari pana ya wima inayopangwa upande wa kulia na kushoto. Kichezaji cha YouTube huweka fremu kwenye video kiotomatiki ili kuhakikisha zinaonyeshwa kwa usahihi, bila kuzipunguza au kuzipanua, pasi na kujali ukubwa wa video au kichezaji. Angalia Usimbaji wa kina ili uone mifano ya video.

    • Ikiwa uwiano halisi wa video ni 1.77:1 na uwiano wa fremu ni 1.77:1 kwa ujumla, teua chaguo la kutenganisha la 16:9 lililo na pikseli za mraba mdogo bila mpaka.
    • Ikiwa uwiano halisi wa video ni 1.77:1 na uwiano wa fremu kwa ujumla si 1.77:1, teua chaguo la kutenganisha la 16:9 lililo na pikseli za mraba mdogo na mpaka wenye rangi moja usiobadilika kadri muda unavyosonga.
    • Ikiwa uwiano halisi wa video ni 1.33:1 na uwiano wa fremu ni 1.33:1 kwa ujumla, teua chaguo la kutenganisha la 4:3 lililo na pikseli za mraba mdogo bila mpaka.
    • Ikiwa uwiano halisi wa video ni 1.33:1 na uwiano wa fremu kwa ujumla si 1.33:1, teua chaguo la kutenganisha la 4:3 lililo na pikseli za mraba mdogo na mpaka wenye rangi moja usiobadilika kadri muda unavyosonga.

    Ikiwa filamu ina toleo la "pan-and-scan" pamoja na toleo halisi la 16:9, pakia matoleo haya mawili kila moja kivyake.

  • Ubora wa video: YouTube inapendelea video za ubora wa juu na kwa ujumla, unapaswa kupakia video yenye ubora wa juu zaidi kadri iwezekanavyo ili iweze kusimbwa na kuchezwa kwa urahisi. Kwa video unazokusudia kuuza au kukodisha, ubora wake haupaswi kuwa chini ya 1920x1080 na uwiano unastahili kuwa 16:9. Kwa maudhui yaliyo au yasiyo na matangazo, YouTube haijabainisha kiwango cha chini zaidi cha ubora lakini inapendekeza ubora wa angalau 1280x720 kwa video ambayo ina uwiano wa 16:9 na ubora wa angalau 640x480 kwa video iliyo na uwiano wa 4:3.

    Unaweza kupakia video za ubora wa chini iwapo hazitaonekana kwa umma kwenye YouTube na ikiwa unazipakia ili zitumike tu kwa marejeleo ya Content ID. Ubora wa video hizi unaweza kuwa "robo moja" - yaani 320x240. Hata hivyo, sharti video ziwe na zaidi ya mistari 200 ili zistahiki kutumika kwa marejeleo.

  • Kasi ya biti ya video: Kwa kuwa kasi ya biti inategemea sana kodeki, hakuna kikomo cha kasi ya chini zaidi kinachopendekezwa. Unapaswa kuboresha kasi ya picha, uwiano na ubora wa video badala ya kasi ya biti. Kwa kawaida, biti 50 au Mbps 80 hutumika kwa video za kuuzwa au kukodishwa.

Ikiwa huwezi kusimba video zako kulingana na vigezo vilivyobainishwa, bado unaweza kuzipakia katika miundo ya .WMV, .AVI, .MOV na .FLV. Katika hali hii, tunapendekeza upakie video ya ubora wa juu zaidi kadri iwezekanavyo. YouTube itakubali maudhui ya video yako kisha itasimba upya faili za video zako inavyohitajika. Hata hivyo, huenda hili likafanya ubora wa video zako usiwe wa juu inavyofaa na likazuia usimbaji wa HQ kwa video zako. Iwapo huwezi kusimba video zako kulingana na vigezo vya muundo vilivyobainishwa, tunapendekeza upakie video chache za majaribio mtandaoni ili uthibitishe kuwa umeridhika na ubora wa video kwenye YouTube.

Mwongozo kuhusu faili za sauti

Mwongozo ufuatayo unahusu nyimbo za sauti unazopakia kwenye YouTube. Mwongozo huu unafafanua vigezo vya muundo vinavyoweka ubora wa juu zaidi wa kucheza faili za sauti kwenye YouTube na kulinganisha nyimbo zako za sauti na zile zinazochezwa katika video zilizopakiwa na watumiaji. Kumbuka, wimbo wa sauti utachezwa tu kwenye YouTube ikiwa umechagua kujumuisha wimbo huo katika mpango wa Ubadilishanaji wa Audio kwenye YouTube. Kwa ujumla, tunapendekeza upakie faili ya sauti yenye ubora wa juu zaidi kadri iwezekanavyo.

  • Aina za faili zinazotumika:
    • Sauti ya MP3 katika metadata ya MP3/WAV
    • Sauti ya PCM katika metadata ya WAV
    • Sauti ya AAC katika metadata ya MOV
    • Sauti ya FLAC
  • Kima cha chini cha kasi ya biti kwa faili za sauti zenye muundo uliobanwa: kbps 64
  • Kima cha chini cha muda unaoweza kusikika: Sekunde 33 (bila kujumuisha hali ya kimya na kelele za mazingira)
  • Kima cha juu cha muda: Hakuna

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
12870828725125058084
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false