Kubuni klipu ya kuangazia

Unapobuni mtiririko mubashara, klipu za kuangazia zinaweza kukusaidia ushiriki toleo fupi lililohaririwa la mtiririko mubashara huku ukitiririsha.

Kuweka alama kwenye mtiririko ili ubuni kwa urahisi klipu ya kuangazia

Ili ubuni klipu za kuangazia kwa urahisi, unaweza kuweka alama kwenye mtiririko  wakati kitu cha kuvutia kinafanyika unapotiririsha mubashara. Kisha unapobuni klipu ya kuangazia katika Kihariri cha YouTube, utaona alama kwenye mtiririko katika ukanda wa wakati.

Jinsi ya kubuni klipu ya kuangazia

Unaweza kutayarisha klipu ya kuangazia unapotiririsha au uihariri baada ya kukamilisha utiririshaji. Ikiwa unatiririsha mwenyewe (kama vile wachezaji wengi), unaweza kuweka alama kwenye mtiririko kwa ajili ya marejeleo na utayarishe klipu ya kuangazia baada ya mtiririko wako kukamilika. Ikiwa wewe ni sehemu ya timu, unaweza kutayarisha klipu ya kuangazia kwa urahisi unapotiririsha.

  1. Fungua Studio ya YouTube.
  2. Upande wa juu kulia, bofya Buni kisha Mubashara.
  3. Bofya Tiririsha au Dhibiti ili uanze kutiririsha.
  4. Ukiona kitu cha kuvutia, weka alama kwenye mtiririko, gusa Weka alama kwenye mtiririko  kutoka sehemu ya juu kulia.
  5. Upande wa juu, bofya Buni klipu ya kuangazia .
  6. Kupunguza video: Chagua unachotaka kuangazia. Unaweza kuburuta vishikio vya pau kwenye ukanda wa wakati au ubadilishe muhuri wa wakati.
  7. Kuzima au kurejesha sauti: Gusa Zima Sauti .
  8. Weka mada, weka mipangilio ya faragha ya video kisha uweke maelezo.
  9. Bofya Anzisha. Video yako itachapishwa kiotomatiki.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7490776809606744198
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false