Tumia mipangilio ya arifa ili udhibiti arifa zako kuhusu shughuli kwenye chaneli yako, ikiwa ni pamoja na majibu na maoni mapya.
Wakati unakagua mipangilio, kumbuka kuwa maoni yanayofuatana kwenye video huenda yasisababishe kutumwa kwa arifa kuhusu kila maoni. Tunakutumia arifa ya mara kwa mara badala yake.
Kudhibiti arifa
Hakikisha kuwa arifa za programu ya Studio ya YouTube na programu ya YouTube zimewashwa kwenye kifaa chako.
- Nenda kwenye Mipangilio
Programu na arifa kwenye kifaa chako.
- Pata YouTube na Studio ya YouTube kwenye orodha ya programu na uhakikishe unawasha arifa.
Kudhibiti arifa za maoni
Programu ya Studio ya YouTube kwenye Android
- Fungua programu ya Studio ya YouTube
.
- Gusa picha yako ya wasifu
.
- Gusa Mipangilio
Arifa za programu
.
- Washa au uzime arifa unazotaka: Maoni, Takwimu, Mafanikio, Sera na Mapato.
Programu ya YouTube kwenye Android
- Fungua programu ya YouTube
.
- Gusa picha yako ya wasifu
.
- Gusa Mipangilio
Arifa.
- Washa au uzime arifa unazotaka.
Kwa maelezo zaidi kuhusu arifa za vifaa vya mkononi, angalia sehemu ya Kudhibiti arifa za YouTube.
Je, huoni maoni?
Huenda usione maoni baada ya kupokea arifa. Sababu za kawaida zinazoweza kufanya usione maoni ni kuwa mtumiaji alifuta maoni yake, au yaliondolewa kwa kukiuka sera.
Huenda usione maoni baada ya kupokea arifa. Sababu za kawaida zinazoweza kufanya usione maoni ni kuwa mtumiaji alifuta maoni yake, au yaliondolewa kwa kukiuka sera.