Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika wanaotumia Kidhibiti Maudhui cha YouTube kudhibiti maudhui yao yaliyo na hakimiliki.
Rekodi za sauti
Aina ya faili inayopendekezwa kwa rekodi za sauti ni FLAC au WAV ambayo haijabanwa. Iwapo huwezi kutoa faili za sauti katika muundo ambao haujabanwa, YouTube pia inakubali faili za MP3 zenye kbps320. YouTube itabadilisha muundo wa faili za sauti kuwa katika miundo mbalimbali ya uwasilishaji; kuwasilisha faili za sauti zilizobanwa kunaweza kusababisha sauti duni kwa mtumiaji.
Kazi ya sanaa ya Albamu
Picha zote za albamu ni lazima ziwe katika muundo wa PNG au JPEG. Ili kuhakikisha ubora mzuri wa mwonekano katika Video za Picha, ni lazima picha iwe ya mraba (uwiano wa urefu na upana wa 1:1) na ukubwa wa juu wa pikseli 4098x4098 na ukubwa wa chini kabisa unaopendekezwa wa 1400x1400 katika DPI 300.