Kujiandaa kupakia faili za DDEX

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika wanaotumia Kidhibiti Maudhui cha YouTube kudhibiti maudhui yao yaliyo na hakimiliki.

Ili uweke mipangilio kwenye akaunti yako kwa ajili ya maudhui yanayopakiwa ya DDEX:

  1. Weka mipangilio kwenye akaunti yako.

    Kabla YouTube haijakubali faili za DDEX kutoka kwako, mwakilishi wako wa washirika anahitaji kuweka mipangilio kwenye akaunti yako ili ikubali faili za DDEX.

    Unahitaji kumpa mwakilishi wako wa washirika Kitambulisho chako cha Mhusika cha DDEX. Ikiwa huna Kitambulisho cha Mhusika cha DDEX, unaweza kujiandikisha ili ukipate katika http://dpid.ddex.net/.

    Ikiwa kwa sasa hupakii maudhui mengi kwa pamoja kwenye YouTube, utahitaji kuwasiliana na mwakilishi wako wa washirika ili akuwekee mipangilio ya kisanduku cha jumla cha SFTP au Aspera.

    Tunapendekeza utumie kisanduku tofauti cha jumla kwa ajili ya uingizaji wa data ya DDEX kando na kile unachotumia kwenye ContentID.

  2. Kuthibitisha na kupakia vikundi vya jaribio.

    Ili utume kikundi cha maudhui yanayopakiwa ya jaribio, weka <MessageControlType> kwenye kichwa cha ujumbe iwe TestMessage kisha unakili faili ya DDEX kwenye kisanduku chako cha jumla. Angalia sehemu ya Kupakia maudhui ili upate maelezo. Baada ya kupakia faili zote za jaribio, unda faili yenye jina linaloanza kwa mfuatano “BatchComplete”, ikifuatiwa na herufi nyingine zozote na kiambishi cha faili cha .xml. Kuwepo kwa faili hii hufahamisha YouTube kwamba kikundi hicho kiko tayari.

    YouTube haipakii ujumbe wa jaribio bali huuthibitisha tu. Huhitaji kujumuisha faili za maudhui unapopakia TestMessage ili uthibitishwe.

    Kutuma vikundi vya jaribio kwa hali zote zinazoruhusiwa na huduma yako:

    Albamu mpya kamili

    Uwasilishaji kamili wa bidhaa wa toleo la albamu ikiwa ni pamoja na faili ya DDEX, faili za sauti, faili za sanaa na masharti ya ofa.

    • Weka <ReleaseType> iwe "Albamu".
    • <ReleaseResourceReferenceList> inapaswa kurejelea nyenzo zote za sauti na sanaa ya albamu zilizowasilishwa.
    Wimbo mpya kamili

    Uwasilishaji kamili wa bidhaa wa toleo la wimbo ikiwa ni pamoja na faili ya DDEX, faili za sauti, faili za sanaa na masharti ya ofa.

    • Weka <ReleaseType> iwe "Wimbo".
    Toleo jipya kamili la diski nyingi

    Uwasilishaji kamili wa bidhaa wa toleo la diski nyingi ikiwa ni pamoja na faili ya DDEX, faili za sauti, faili za sanaa na masharti ya ofa.

    • Weka <ReleaseType> iwe "Albamu".
    • Toleo kuu linapaswa kuwa na <ResourceGroup> nyingi, kila moja ikiwa na <SequenceNumber>, inayoambatana na diski hizo nyingi.
    Sasisho kamili

    Sasisho kamili lenye faili mpya za sauti au picha pamoja na faili ya DDEX iliyosasishwa.

    • Sasisha kitambulisho cha ujumbe na muhuri wa wakati.
    • Toa masasisho ya metadata ya ziada inavyohitajika.
    Kusasisha metadata ya wimbo

    Sasisho la metadata pekee, faili za maudhui zikiwa hazijajumuishwa wala kurejelewa kwenye faili ya DDEX.

    YouTube inaruhusu tu masasisho kamili ya metadata. Ni sharti ujumuishe metadata yote ya wimbo, ikiwa ni pamoja na thamani ambazo hazijabadilika.
    • Futa sehemu ya <TechnicalSoundRecordingDetails> na <TechnicalImageDetails> ya kila nyenzo, kwa sababu faili hizo hazijumuishwi.
      Kosa la kawaida ni kuondoa kipengee chote cha <Image> badala ya kuondoa tu sehemu ya <TechnicalImageDetails> iliyopo na kuondoa marejeleo yote ya sehemu hiyo. Hali hii husababisha athari isiyofaa ya kuondoa sanaa ya albamu kutoka kwenye albamu kabisa.
    Kutenganisha masharti ya ofa

    Uwasilishaji wa toleo wenye awamu mbili. Uwasilishaji wa kwanza hujumuisha faili ya DDEX, faili za sauti na faili za sanaa, bila masharti ya ofa. Uwasilishaji wa pili hutoa masharti ya ofa.

    • Uwasilishaji wa kwanza unajumuisha faili za maudhui lakini uwasilishaji wa pili hauna faili hizo.
    Kuweka wimbo mpya kwenye albamu

    Tuma sasisho lenye data ya wimbo mpya na ambalo linaweka wimbo huo kwenye <Release> inayofaa.

    • Weka vipengee vya <SoundRecording>, <Release> na <ReleaseDeal> vya wimbo mpya.
    • Weka wimbo kwenye kipengee kikuu cha <Release> cha albamu, kwenye sehemu za <ReleaseResourceReferenceList> na <ResourceGroup> zinazobainisha mfuatano wa wimbo kwenye albamu.
    • Wasilisha upya nyimbo zote, si wimbo mpya pekee.

    Ujumbe wa jaribio ukithibitishwa bila makosa, badilisha <MessageControlType> iwe LiveMessage, pakia faili za maudhui zinazohusishwa kisha urudie mchakato wa kupakia.

  3. Kukagua vikundi vya jaribio.

    Baada ya kupakia vikundi vya jaribio, shirikiana na mwakilishi wako wa washirika ili kukagua vipengee husika. Usiporidhishwa na matokeo, fanya marekebisho yanayohitajika kisha urudie jaribio.

  4. Jaribio kamili la mwanzo hadi mwisho.

    Baada ya kuona kuwa vikundi vyako vya jaribio ni sahihi, wasilisha takriban matoleo 200 kwa ajili ya jaribio la mwanzo hadi mwisho.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6943328770700426249
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false