Tazama filamu na vipindi vya televisheni vyenye ubora wa HD au 4K kwenye YouTube

Kila filamu kwenye YouTube na Vipindi vya televisheni vinapatikana katika ubora wa kawaida. Tunatoa baadhi ya maudhui katika ubora wa juu (HD) au Ubora wa Juu Zaidi (UHD) wa 4K. Makubaliano yetu ya leseni ya Studio yanasema iwe uchezaji wa HD au UHD unapatikana kwenye kifaa. Tunajitahidi kupanua upatikanaji wa maudhui yaliyo na ubora wa HD na UHD katika vifaa vyako vyote unavyopenda.

Kumbuka:
  • Wakati mwingine, unaweza kununua au kukodisha toleo la HD/UHD la video kwenye kifaa au kivinjari ambacho hakiruhusu uchezaji wa HD/UHD. Bado unaweza kutazama maudhui katika ubora wa chini kwenye kifaa hicho, au kutazama katika ubora wa HD/UHD ukitumia kifaa tofauti kinachoruhusiwa.

Je, HD ni nini?

HD (au Ubora wa Juu) inarejelea video ya ubora wa juu kuliko SD (au Ubora wa Wastani). Kwenye HD, picha itakuwa na ung'aavu zaidi kuliko kwenye SD. Kwenye YouTube, HD inamaanisha video ina mistari 720–1080 ya ubora wa wima. Inaonyeshwa kama 720p au 1080p kwenye mipangilio ya ubora ya kichezaji cha YouTube. Kwa kulinganisha, 360 au 480, ni ya ubora wa kawaida kwa SD.

Je, UHD ni nini?

UHD wa 4K (au Ubora wa Juu Zaidi) inarejelea ubora wa juu zaidi wa video kuliko HD. Kwenye UHD, picha itakuwa nzuri zaidi kuliko HD. Kwenye YouTube, UHD inamaanisha kuwa video ina mistari 2160–3840 ya ubora wa wima (ikilinganishwa na 720 au 1080, ambazo ni za ubora wa kawaida kwa HD). Unaweza kupata maelezo ya ubora wa video ndani ya kichezaji cha video ya YouTube.

Kutazama video zenye ubora wa HD kwenye YouTube

Ikiwa video inapatikana katika ubora wa HD, unaweza kuchagua Mipangilio kisha ubadilishe ubora. Ikiwa video haipatikani katika ubora wa HD, video yako itacheza katika ubora wa SD badala yake.

Kila inapopatikana, unaweza kutazama video za ubora wa HD ukitumia toleo jipya zaidi la YouTube kwenye:

  • iPhone na iPad
  • Vifaa vingi vya Android vyenye uwezo wa HD
  • Baadhi ya televisheni zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti, yaani zilizoundwa 2013 na miaka ya baadaye
  • Android TV/Google TV
  • Chromecast
  • Apple TV
  • Xbox One na matoleo mapya zaidi
  • PlayStation 3 na matoleo mpya zaidi
  • Roku

Kutazama video zenye ubora wa 4K UHD kwenye YouTube

Unaweza kutazama video zenye ubora wa 4K UHD ulizonunua kwa kutumia programu ya YouTube kwenye televisheni zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti na Android TV inayotimiza vigezo au kwa kutumia Chromecast Ultra.

Uchezaji wa UHD unahitaji muunganisho wa intaneti yenye kasi zaidi kuliko video za HD au SD kwani YouTube inahitaji kutiririsha data nyingi zaidi. Ili kutiririsha video zenye ubora wa UHD, utahitaji kasi thabiti ya kupakua ya angalau megabiti 15 kwa sekunde. Bila kipimo data thabiti, filamu yako inaweza kucheza katika ubora wa HD au SD.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
7611596904542043412
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false