Kwenye baadhi ya programu na vifaa vya zamani (kama vile toleo la zamani la programu ya YouTube), unaweza kuona ujumbe wa "Kitendo hiki hakiruhusiwi" unapojaribu kufungua chaneli.
Hali hii ikitokea, inamaanisha kuwa programu yako ya YouTube imepitwa na wakati. Unaweza kujaribu mojawapo ya chaguo hizi ili ufungue chaneli yako:
- Sasisha ili upate toleo jipya zaidi la programu yako ya YouTube na ujaribu tena kufungua chaneli mpya.
- Ukitumia kompyuta, fungua chaneli mpya kwenye YouTube ukitumia kivinjari. Kisha, ingia katika chaneli ukitumia programu kwenye kifaa chako cha mkononi.