Ikiwa wewe ni mmiliki wa orodha, unaweza kufanya orodha yako iwe ya umma, ya faragha au ambayo haijaorodheshwa.
Vidokezo
- Huenda kipengele hiki kisitumike kwenye matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube.
- Kuna kikomo cha idadi ya orodha za video za umma ambazo chaneli inaweza kutayarisha kila siku katika YouTube Music, programu kuu ya YouTube na API ya YouTube. Unaweza kuongeza kikomo chako cha kila siku kwa kupata ufikiaji wa vipengele vya kina. Pata maelezo zaidi.
Kuweka mipangilio ya faragha ya orodha kupitia Studio ya YouTube
- Ingia katika Studio ya YouTube.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui Orodha.
- Kwenye orodha ambayo ungependa kusasisha, bofya Maelezo .
- Kwenye ukurasa wa “Maelezo ya orodha”, bofya Uonekanaji chagua mipangilio mipya ya faragha katika menyu kunjuzi.
- Bofya Hifadhi.
Kuweka mipangilio ya faragha ya orodha kupitia YouTube
- Ingia katika YouTube.
- Nenda kwenye kichupo cha Wasifu Orodha .
- Chagua Angalia orodha kamili chini ya orodha ambayo ungependa kubadilisha.
- Chini ya jina la orodha, chagua mipangilio mipya ya faragha kwenye menyu kunjuzi.
Mipangilio ya faragha
- Mtu yeyote anaweza kutazama na kushiriki video na orodha za kucheza za Umma .
- Mtu yeyote aliye na kiungo cha video anaweza kutazama na kutuma video pamoja na orodha ambazo Hazijaorodheshwa.
- Mifumo ya YouTube na wahakiki wanadamu wanaweza kukagua video na orodha za Faragha ili kubaini ufaafu wa kuwekwa matangazo, hakimiliki na mbinu nyingine za kuzuia matumizi mabaya.
Kipengele | Haijaorodheshwa | Faragha | Umma |
---|---|---|---|
Unaweza kushiriki URL | Ndiyo | Hapana | Ndiyo |
Inaweza kuwekwa katika sehemu ya kituo | Ndiyo | Hapana | Ndiyo |
Inaonekana katika utafutaji, video zinazohusiana na rekodi | Hapana | Hapana | Ndiyo |
Imechapishwa kwenye chaneli yako | Hapana | Hapana | Ndiyo |
Inaonekana katika mipasho ya Wanaofuatilia | Hapana | Hapana | Ndiyo |