Ikiwa wewe ni mmiliki wa orodha ya video, unaweza kufanya orodha yako ya video iwe ya umma, ya faragha au ambayo haijaorodheshwa kama tu unavyoweza kufanya kwenye video mahususi.
Kumbuka: Huenda kipengele hiki kisipatikane kwa matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube. Pata maelezo zaidi.
Kuweka mipangilio ya faragha ya orodha ya video kupitia Studio ya YouTube
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Orodha za video .
- Karibu na orodha ya video ambayo ungependa kusasisha, bofya Badilisha katika YouTube .
- Chini ya jina la orodha ya video, bofya menyu kunjuzi ya faragha ya Orodha ya video.
- Chagua mipangilio mipya ya faragha.
- Bofya Hifadhi.
Kuweka mipangilio ya faragha ya orodha ya video kupitia YouTube
- Nenda kwenye kichupo cha Wasifu ili uangalie orodha zako zote za video.
- Chagua orodha ya video ambayo ungependa kubadilisha.
- Chini ya jina la orodha ya video, bofya menyu kunjuzi ya faragha ya Orodha ya video.