Kipakiaji cha Vifurushi hukuwezesha kupakia metadata, rekodi za sauti, na faili nyingi za video kwa haraka kwenye YouTube. Ina kiolesura kinachokuwezesha kuburuta na kudondosha faili unazotaka kupakia. Ili kuunda vipengee vipya au kusasisha vilivyopo, unahitaji kupakia faili ya metadata (lahajedwali au faili ya DDEX ) pamoja na faili za maudhui za vipengee vyote.
Ili upakie faili ukitumia Kipakiaji cha Vifurushi:
- Ingia katika Kidhibiti Maudhui cha Studio.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Masasisho ya maudhui .
- Iwapo hujawahi kutumia kipengele chochote cha Uwasilishaji wa Maudhui, YouTube itakufungulia kiotomatiki akaunti ya mpakiaji. Unaweza kubadilisha anwani ya barua pepe au chaneli chaguomsingi ya mpakiaji katika ukurasa wa Mipangilio kwenye Akaunti za aliyepakia.
- Kwenye kona ya juu, bofya Thibitisha kisha Upakie.
- Weka faili ambazo ungepanda kuzipakia. Unaweza kuziweka faili kwa njia mbili:
-
Buruta faili kwenye kompyuta yako kisha uzidondoshe kwenye orodha ya faili katika kivinjari chako.
-
Bofya Chagua faili kisha uteue faili ambazo ungependa kuzipakia.
-
Ni lazima orodha ya faili ijumuishe faili moja ya metadata inayotumika, inaweza kuwa faili ya lahajedwali au ya DDEX.
-
-
Baada ya kuwekwa, faili ya metadata itaanza kiotomatiki mchakato wa uthibitishaji. Iwapo hitilafu zitapatikana kwenye metadata, utahitaji kuzirekebisha kisha uithibitishe faili tena.
-
Ikihitajika, weka faili zote za sauti na video kwenye kifurushi kwa kubofya Weka faili.
- Bofya Chakata kifurushi.
- Kulingana na idadi na ukubwa wa faili ulizopakia na uchangamano wa mabadiliko, inaweza kuchukua saa au dakika kadhaa kukamilisha upakiaji wa vipengee vingi.