Kuunganisha kwenye Kisanduku chako cha jumla cha Aspera

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika wanaotumia Kidhibiti Maudhui cha YouTube kudhibiti maudhui yao yaliyo na hakimiliki.

Baada ya kuweka mipangilio ya kisanduku chako cha jumla, unahitaji kuunda muunganisho unaoweza kutumika tena kati ya kiteja cha Aspera na kisanduku chako cha jumla.

Hakikisha una jina la kisanduku cha jumla na anwani ya IP mkononi kwa marejeleo rahisi; unaweza kupata maelezo haya chini ya Akaunti za Aliyepakia katika menyu ya Mipangilio iliyo upande wa kushoto.

Ili kuunda muunganisho wa Aspera:

  1. Fungua programu yako ya kiteja cha Aspera.

  2. Bofya aikoni ya Miunganisho ili ufungue Kidhibiti cha Muunganisho.

  3. Bofya + ili uweke muunganisho mpya.

  4. Weka jina la mpangishaji la kisanduku chako cha jumla kilichotolewa na mwakilishi wa mshirika wako kwenye kisanduku cha maandishi cha Seva pangishi. Jina la mpangishaji linapaswa kuwa mojawapo ya yafuatayo na lilingane na eneo lako la kijiografia:

    • us.aspera.googleusercontent.com

    • eu.aspera.googleusercontent.com

    • asia.aspera.googleusercontent.com

  5. Weka jina la kisanduku cha jumla katika kisanduku cha maandishi cha Mtumiaji. Ni lazima lianze na "asp-"

  6. Chagua Ufunguo wa Umma kama chaguo la uthibitishaji, kisha uchague kitufe cha kisanduku hiki cha jumla kutoka kwenye orodha ya funguo zinazopatikana.

  7. Bofya kitufe cha Ya Kina ili kuonyesha Mipangilio ya Kina ya Muunganisho.

  8. Badilisha thamani ya Mlango wa SSH (TCP) kuwa 33001.

  9. Bofya SAWA mara mbili ili uhifadhi mabadiliko yako kisha urudi kwenye skrini kuu ya kiteja cha Aspera.

    Muunganisho wako mpya huonekana upande wa kulia wa skrini.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13229159889101022659
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false