Kuweka mipangilio ya kisanduku chako cha jumla

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika wanaotumia Kidhibiti Maudhui cha YouTube kudhibiti maudhui yao yaliyo na hakimiliki.

Baada ya mwakilishi wako wa washirika kubuni kisanduku chako cha jumla, unahitaji kuweka mipangilio chaguomsingi ya akaunti yako.

Ili uweke mipangilio ya kisanduku chako cha jumla:

  1. Ingia katika akaunti ya Kidhibiti Maudhui cha YouTube

  2. Bofya Akaunti za wanaopakia katika menyu ya kushoto ya Mipangilio.

  3. Rekodi jina na anwani ya kisanduku cha jumla.

    Utahitaji maelezo haya ili kuunganisha kwenye kisanduku cha jumla.

    Kwa Visanduku vya jumla vya Aspera, jina huanza kwa asp-; kwa SFTP dropbox, jina huanza kwa yt-. Anwani ya kisanduku cha jumla cha Aspera huonyeshwa kama Anwani ya Seva; anwani ya SFTP dropbox ni partnerupload.google.com.

    Akaunti zilizo na wamiliki wengi wa maudhui zinaweza kuwa na zaidi ya kisanduku kimoja cha jumla. Hakikisha kuwa unarekodi maelezo ya kisanduku chako cha jumla.
  4. Thibitisha kuwa Kituo Chaguomsingi na Funguo za Umma za SSH ni sahihi.

    Mtumiaji chaguomsingi wa YouTube atatambua akaunti (kituo) ambayo itachaguliwa kama mmiliki wa video unazopakia iwapo mipasho ya maudhui haibainishi mmiliki tofauti.

    Kisanduku cha Funguo za Umma za SSH kinapaswa kuwa na ufunguo wa SSH uliotoa kwa mwakilishi wako wa washirika. Hakikisha kuwa ufunguo huo unajumuisha anwani yako ya barua pepe mwishoni.

  5. Katika kisanduku cha maandishi cha Barua Pepe za Taarifa, weka anwani moja au zaidi za barua pepe ambako ungependa YouTube itume ripoti za hali.

    Weka anwani nyingi za barua pepe, moja kwa kila mstari.  Bofya Hifadhi.

Tafadhali kumbuka kuwa kisanduku cha jumla hulingana na mmiliki wa maudhui wala si kituo. Yaani, unaweza kupakia kwenye vituo mbalimbali kwa kutumia kisanduku kimoja tu cha jumla.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7661991008960913082
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false