Matatizo ya kutumia zana za wengine na Akaunti za Biashara

Hatua ya kuunganisha vituo vyako kwenye Akaunti za Biashara inakuwezesha kubadilisha vituo kwenye akaunti moja. Kwa bahati mbaya, baadhi ya programu za wengine na programu za zamani haziruhusu ubadilishaji wa akaunti. Zinaweza kuleta ujumbe wa hitilafu au kuingia katika akaunti ya kituo ambacho si sahihi. Hili linaweza kutokea kwenye:

  • Programu ya iOS Photos
  • Baadhi ya programu za zamani za vifaa vya mkononi
  • Baadhi ya vifaa vya kawaida na vifaa vya michezo ya video
  • Programu ya kuhariri kama vile iMovie au Premiere
  • Zana kama vile Wirecast
  • Programu nyingine zinazotumia uthibitishaji wa API

Jaribu moja ya hatua zilizo hapa chini ili kutatua tatizo hilo:

  • Hakikisha unaingia katika akaunti ukitumia anwani ya barua pepe na nenosiri la Akaunti yako ya Google.
  • Hakikisha unatumia toleo jipya zaidi la programu yako.
  • Ikiwa hatua hizi hazitatui tatizo hilo, angalia hapa chini.

Kuchagua kituo ambako utatumia programu za wengine

Weka kituo chaguomsingi kwenye akaunti yako ili uchague kituo ambacho kitateuliwa utakapoingia katika akaunti ya programu ambazo haziruhusu ubadilishaji wa kituo.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
15905640381904958606
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false