Kuthibitisha metadata

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika wanaotumia Kidhibiti Maudhui cha YouTube kudhibiti maudhui yao yaliyo na hakimiliki.

Hakikisha unathibitisha faili yako ya DDEX au lahajedwali kabla ya kuipakia. Hitilafu zozote zilizo kwenye faili yako ya CSV au DDEX zitaripotiwa wakati wa hatua hii na inaweza kuzuia hitilafu wakati wa kupakia. Hatua hii inaweza kusaidia zaidi katika kuthibitisha data inayozalishwa kiotomatiki au msimbo maalum unaozalisha faili ya CSV au DDEX.

Ili uthibitishe faili ya metadata:

  1. Bofya kitufe cha Thibitisha na Upakie kinachoonekana chini ya UWASILISHAJI WA MAUDHUI kwenye upande wa kushoto wa menyu ya Studio ya YouTube.
  2. Ili uthibitishe, bofya CHAGUA FAILI na uchague faili ya kuthibitisha.  Unaweza pia kubofya na kuburuta faili zilizo kwenye kompyuta yako uzipeleke kwenye dirisha la kivinjari.

    Orodha ya faili lazima ijumuishe faili moja ya metadata inayotumika, inaweza kuwa ya faili ya lahajedwali au DDEX. Baada ya kuweka, faili ya metadata kiotomatiki itaanza hatua ya kuthibitisha (aikoni inayozunguka itaonekana.)
     
  3. Kagua hitilafu (ikiwa zipo) kwa kubofya kitufe kilicho karibu na aikoni nyekundu.

    Badilisha metadata kwenye faili halisi. Ukimaliza, weka tena faili kwenye ukurasa wa Aliyepakia. Iwapo jina la faili halibadilki, YouTube itatumia toleo jipya zaidi la faili na itaanzisha upya hatua ya uthibitishaji.
    • Ikiwa faili yako inasasisha data pekee, ikimaanisha, iwapo haijumuishi faili zozote za video au sauti , unaweza kubofya Chakata kifurushi ili utume kifurushi kichakatwe.
    • Iwapo kifurushi chako kinahitaji faili za video au sauti na upo tayari kupakia, weka faili hizi za ziada kwenye kifurushi na usubiri hatua ya uthibitishaji ikamilike.  Bofya Chakata kifurushi ili utume kifurushi kichakatwe.
    • Ikiwa unathibitisha tu faili ya metadata na bado hauko tayari kupakia, unaweza kuondoa kifurushi hicho kwa kubofya kitufe cha Futa rasimu .

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
15709497682144891737
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false