Video zenye manukuu zitakuwa na maandishi ya “CC” chini ya muhtasari wa video kwenye matokeo ya utafutaji. Ikiwa ungependa matokeo ya utafutaji yaonyeshe video zenye manukuu pekee, washa kichujio hiki cha utafutaji:
- Weka maneno yako muhimu kwenye upau wa kutafutia wa YouTube kisha ubofye Tafuta .
- Bofya Vichujio .
- Bofya Manukuu/CC.