Kuingia katika akaunti ya programu ya YouTube katika televisheni inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kifaa cha michezo ya video

Ingia katika akaunti ya programu ya YouTube ili utumie vipengele kama vile kutazama maudhui yanayolipiwa, kufuatilia vituo na kuangalia Maktaba yako.

Baada ya kuingia katika akaunti, unaweza kuvinjari maudhui mbalimbali ya programu ya YouTube kwenye televisheni inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kifaa chako cha michezo ya video. Unaweza pia kuunganisha kifaa chako kwenye televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti na kutumia simu au kishikwambi chako kama kidhibiti cha mbali.

Kumbuka:

Jinsi ya Kuingia Kwenye YouTube katika Televisheni Yako

Kuanza mchakato wa kuingia katika akaunti kwenye televisheni inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kifaa chako cha michezo ya video

  1. Ili uanze, fungua programu ya YouTube kwenye televisheni au kifaa chako cha michezo ya video. Ikiwa bado hujaisakinisha, pakua programu ya YouTube katika duka la programu kwenye televisheni au kifaa chako cha michezo ya video.
  2. Nenda kwenye menyu ya kushoto.
  3. Chagua Ingia katika akaunti .

Unaweza kuingia katika akaunti ya YouTube ukitumia simu, televisheni au kivinjari chako.

Endelea na mchakato wa kuingia katika akaunti ukitumia simu yako

Kidokezo: Chaguo la kuingia katika akaunti ukitumia simu yako linapatikana tu kwenye vifaa mahususi. Ikiwa huwezi kuingia katika akaunti ukitumia simu yako, jaribu kuingia katika akaunti kwenye televisheni au ukitumia kivinjari.
  1. Hakikisha kuwa kifaa chako cha mkononi kinatumia mtandao wa Wi-Fi unaotumiwa na televisheni yako.
  2. Chagua Ingia katika akaunti ukitumia simu yako.
  3. Fungua programu ya YouTube kwenye simu yako.
  4. Fuata maelekezo ya kuingia katika akaunti kwenye televisheni yako.

Endelea na mchakato wa kuingia katika akaunti kwenye televisheni yako

Kidokezo: Ikiwa huwezi kuingia katika akaunti ukitumia televisheni yako, jaribu kuingia katika akaunti ukitumia simu au kivinjari chako.
  1. Chagua Ingia katika akaunti ukitumia televisheni yako.
  2. Tumia kibodi kuweka barua pepe au nambari yako ya simu ya Akaunti yako ya Google.
  3. Bofya Endelea.
  4. Tumia kibodi kuweka nenosiri la Akaunti yako ya Google.
  5. Thibitisha akaunti yako.

Endelea na mchakato wa kuingia katika akaunti ukitumia kivinjari

Kidokezo: Ikiwa huwezi kuingia katika akaunti ukitumia kivinjari, jaribu kuingia katika akaunti kwenye televisheni yako au ukitumia simu yako.
  1. Chagua Ingia katika akaunti ukitumia kivinjari.
  2. Msimbo utaonyeshwa kwenye televisheni yako.
  3. Kwenye simu, kompyuta kibao au kompyuta yako, fungua kivinjari na uende kwenye youtube.com/tv/activate.
  4. Weka msimbo ulioonyeshwa kwenye televisheni yako.
  5. Ingia katika akaunti yako.

Kutumia akaunti tofauti kwenye televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kwenye kifaa cha michezo ya video

Kwenye programu ya YouTube kwenye televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kifaa cha michezo ya video, unaweza kuingia katika akaunti tofauti na kubadili akaunti hizi kwa urahisi. Wanafamilia wako wanaweza kuweka akaunti zao na wageni wanaweza kutumia YouTube bila kuingia katika akaunti (matumizi ya wageni). Hali ya matumizi ya wageni huwawezesha wengine watumie YouTube kwenye televisheni yako au kifaa cha michezo ya video bila kuingia katika akaunti. Vitendo vyovyote vinavyofanywa bila kuingia katika akaunti katika hali ya matumizi ya wageni havitaathiri maudhui yanayopendekezwa kwenye akaunti yako.

Kumbuka: Ukichagua wasifu wa mtoto wako au wasifu wa mgeni kwenye YouTube Kids, utaingia katika YouTube Kids. Pata maelezo zaidi kuhusu hali hii ya utumiaji.

Kuongeza Akaunti nyingine ya Google kwenye kifaa cha michezo ya video au televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti

Ili uongeze akaunti nyingine katika programu ya YouTube kwenye kifaa cha michezo ya video au televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti:

  1. Fungua programu ya YouTube kwenye televisheni au kifaa chako cha michezo ya video.
  2. Ikiwa programu itafunguka na kukuuliza “Ni Nani Anayetazama?” teua chaguo husika:
    1. Hali ya mgeni: Hukuwezesha kutumia YouTube ukiwa umeondoka katika akaunti.
    2. YouTube Kids: Humuwezesha mtoto wako kutumia YouTube Kids akiwa ameondoka katika akaunti. Chaguo hili litatokea tu ikiwa umeweka mipangilio ya wasifu wa mgeni kwenye YouTube Kids.
    3. Weka akaunti: Hukuwezesha kuingia katika akaunti yako.
    4. Weka wasifu wa YouTube Kids wa mtoto wako: Hukuwezesha kuingia katika wasifu wa YouTube Kids wa mtoto wako.
  3. Kama programu itafunguka ikiwa imeingia katika akaunti:
    1. Nenda kwenye menyu ya kushoto.
    2. Katika sehemu ya juu, chagua picha yako ya wasifu.
    3. Kwenye kichupo cha Akaunti, teua chaguo linalofaa:
      1. Hali ya mgeni: Hukuwezesha kutumia YouTube ukiwa umeondoka katika akaunti.
      2. Ongeza akaunti: Huwawezesha wanafamilia wengine waongeze akaunti zao. Unaweza kuingia katika akaunti ya YouTube ukitumia televisheni au kifaa chako binafsi.
      3. Weka mipangilio ya YouTube Kids: Hukuwezesha kuweka mipangilio ya wasifu wa mgeni wa YouTube Kids ambayo mtoto wako anaweza kutumia akiwa ameondoka katika akaunti.

Switch between signed in Google Accounts on your smart TV or game console

You can easily switch between signed in accounts on your smart TV or game console.

Note: You can only switch between accounts after you’ve added the account on your smart TV or game console. If you need to add an account, use the instructions above and then use the instructions here to switch between accounts.

To switch between signed in accounts in the YouTube app on your smart TV or game console:

  1. Open the YouTube app on your TV or game console.
  2. If the app opens:
    1. Asking you “Who’s Watching?”:
      1. Select the account you’d like to use for YouTube.
    2. Already signed in to an account:
      1. Go to the left-hand navigation.
      2. At the top, select the profile picture.
      3. Within the Accounts tab, select the account you’d like to use for YouTube.

Kutatua matatizo ya kuingia katika akaunti kwenye televisheni inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kifaa chako cha michezo ya video

Ikiwa unatatizika kuingia katika YouTube ukitumia Akaunti yako ya Google, unaweza kupata usaidizi wa kuingia katika akaunti.

Huwezi kuingia katika akaunti ya YouTube moja kwa moja kupitia vifaa vya Chromecast vya zamani. Unaweza kudhibiti kipindi chako cha kutuma maudhui kwenye simu yako ukiwa umeingia katika akaunti kupitia simu yako. Kwa kutumia kidhibiti cha mbali, unaweza kutumia programu ya YouTube bila kuingia katika akaunti.

Ili utekeleze vitendo kwenye video (kama vile kupenda video au kufuatilia watayarishi), endelea kutumia kifaa chako cha mkononi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7710561088586272230
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false