Kipengele cha SSL

Kwa kutegemea kama mtu ameingia au ameondoka katika akaunti, kurasa za YouTube zinaweza kupakiwa kupitia muunganisho salama au usio salama. Miunganisho salama hufanyika kupitia SSL. Ili kuzuia ujumbe wa tahadhari kwenye kivinjari cha mtazamaji, tunahitaji matangazo, faili za matangazo na vipengee vya ufuatiliaji viombwe kwa kutumia muunganisho unaofaa:

  • Kwenye kurasa zisizo salama (HTTP://), tangazo, faili ya tangazo na pikseli za ufuatiliaji zinaweza kutumia HTTP au HTTPS.
  • Kwenye kurasa salama (HTTPS://), ni lazima tangazo, faili ya tangazo na pikseli za ufuatiliaji zitumie HTTPS pekee. Pia, kwa matangazo na faili za matangazo zinazopakiwa kwa kutumia HTTPS://, ni lazima maombi yote yanayofuatia ya vipengee vya maudhui au URL za ufuatiliaji yatumie HTTPS://. Faili zote za matangazo ni lazima ziweze kuwasilisha kupitia HTTP na HTTPS bila kuhitaji uelekezaji maalum wa vyanzo vya wanaoona tangazo. Ikiwa URL za pikseli za ufuatiliaji zimetolewa, ni lazima zitii masharti ya SSL (zianze kwa HTTPS://). Sehemu ya pekee ya tangazo inayoruhusiwa kutotii masharti ya SSL ni URL ya kubofya (ukurasa wa kutua unaolengwa).

Maelezo zaidi

Matangazo yenye maudhui anuai yanayotolewa na wengine

Baadhi ya watoa huduma husahihisha kiotomatiki faili yao ya matangazo ili itii masharti ya SSL. Ukitumia watoa huduma hawa, unahitaji kufanya mabadiliko madogo sana ili faili yako ya tangazo itii masharti ya SSL. Orodha ya watoa huduma na vipengele vyao inapatikana hapa.

Pikseli za ufuatiliaji za VAST

Kwa ajili ya ufuatiliaji wa matangazo ya VAST kama vile ya ndani ya Mtiririko na ndani ya Video, tutaomba URL zozote zisizo salama kupitia muunganisho salama. Tutafaulu kufanya hivi kwa kuondoa HTTP:// na kuweka HTTPS:// badala yake kabla ya kuomba URL husika. Ikiwa mtoa huduma wako wa ufuatiliaji hatumii kipengele hiki, URL ya ufuatiliaji inayotolewa ni lazima itii masharti ya SSL (ianze kwa HTTPS://). Orodha ya watoa huduma na vipengele vyao inapatikana hapa.

Matangazo ya VAST yanayotolewa na wengine

Matangazo yote ya VAST yanayotolewa na wengine ni lazima yatii masharti ya SSL. URL yoyote ndani ya jibu la VAST ni lazima itumie muunganisho unaofaa.

  • Kwenye kurasa zisizo salama (HTTP://), faili ya tangazo na pikseli za ufuatiliaji zinaweza kutumia HTTP au HTTPS.
  • Kwenye kurasa salama (HTTPS://), ni lazima faili ya tangazo na pikseli za ufuatiliaji zitumie HTTPS pekee. Wakati mwingine, mtoa huduma wako hatasahihisha kiotomatiki jibu la tangazo litumie itifaki inayofaa au hataondoa HTTP:// na kuweka HTTPS:// badala yake. Katika hali hizi, ni lazima maudhui na URL zote za ufuatiliaji katika tangazo la VAST zitumie HTTPS:// kwa chaguomsingi.

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11837441045081936019
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false