Kudhibiti mipangilio ya chaneli

Unaweza kudhibiti mipangilio ya chaneli yako katika Studio ya YouTube. Badilisha kila kitu kuanzia nchi au eneo uliko hadi uonekanaji wa chaneli yako.

  1. Ingia katika Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Mipangilio kisha Chaneli.
  3. Rekebisha mipangilio ya chaneli.
  4. Bofya Hifadhi.

picha ikionyesha jinsi ukurasa wa mipangilio ya chaneli unavyoonekana

Maelezo ya msingi

Nchi unakoishi
Unaweza kuchagua nchi au eneo la chaneli yako ya YouTube kwa kutumia Kishale cha chini . Kutimiza masharti ya kujiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube kunategemea mipangilio ya nchi au eneo unayochagua hapa.
Maneno muhimu
Unaweza kuweka maneno muhimu yanayohusiana na chaneli yako kupitia mipangilio hii.

Mipangilio ya kina

Hadhira
Rahisisha utaratibu wako kwa kubainisha hadhira ya chaneli au video zako. Mipangilio hii itaathiri video zilizopo na utakazopakia siku zijazo.
Ukichagua kutobainisha hadhira, utapata vikwazo fulani na utahitajika kubainisha video ambazo zinalenga watoto kwenye chaneli yako.

Kuruhusu maarifa kuhusu chaneli yafikiwe

Watayarishi walio katika Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) wanaweza kuongeza fursa za mapato kutoka kwenye matangazo, ufadhili wa kibiashara na mipango ya washirika wa ununuzi kwa kuruhusu takwimu za chaneli, demografia za hadhira na maarifa kuhusu utendaji wa ununuzi (ikiwa uko katika Mpango wa washirika wa Ununuzi kwenye YouTube) ufikiwe na watangazaji wengine, chapa na mifumo. Mipangilio hii huwa imezimwa kwa chaguomsingi na una udhibiti kamili wa kuwasha au kuzima kipengele cha kuruhusu maarifa kuhusu chaneli yafikiwe wakati wowote.
Kuunganisha akaunti ya Google Ads
Unaweza kuunganisha chaneli yako ya YouTube na akaunti ya Google Ads ili uruhusu matangazo yaonyeshwe. Matangazo haya ni kulingana na jinsi video za chaneli yako zinavyotazamwa na hukuwezesha kufikia maarifa.
Manukuu ya kiotomatiki
Wakati mwingine kipengele cha Manukuu ya kiotomatiki hukosea. Ukichagua kisanduku cha “Usionyeshe maneno ambayo huenda hayafai”, unaweza kuzuia maneno ambayo huenda hayafai yasionyeshwe kwenye video zako.
Matangazo
Ukiteua chaguo hili, matangazo yaliyowekewa mapendeleo kulingana na mambo yanayowavutia watazamaji au matangazo ya kutangaza tena yatazimwa. Kuzima mipangilio hii kunaweza kupunguza mapato ya chaneli yako. Isitoshe, ripoti za vitendo vilivyopatwa na orodha za kutangaza tena zitaacha kufanya kazi kwenye chaneli yako.
Klipu
Chaguo la "Ruhusu watazamaji watayarishe klipu kutokana na maudhui yangu" huwaruhusu watazamaji wako watayarishe klipu kutokana na maudhui yako. Ukiacha kuteua chaguo hili, klipu zilizopo za maudhui yako zitazimwa. Vivyo hivyo, kuteua chaguo hili kutawasha tena klipu zilizopo za maudhui yako.
Kuelekeza kwenye chaneli nyingine

Unaweza kutumia toleo lililofupishwa la URL maalum ili kuelekeza hadhira yako kwenye chaneli nyingine. Katika sehemu ya Kiungo Kinachoelekeza Kwingine, weka URL ya tovuti ambako kiungo chako kinachoelekeza kwingine kinapaswa kuelekeza.

Kumbuka: Viungo vinavyoelekeza kwingine vinapatikana kwa washirika na watangazaji ambao wamewasha kipengele hiki kupitia msimamizi wao wa washirika au mwakilishi wao wa mauzo.

Kwa mfano, iwapo URL yako ni www.youtube.com/c/YouTubeCreators, unaweza kufanya URL yako iliyofupishwa (www.youtube.com/YouTubeCreators) iwaelekeze watazamaji kwenye chaneli ya YouTube Nation kwa kuweka www.youtube.com/user/youtubenation au www.youtube.com/channel/UCUD4yDVyM54QpfqGJX4S7ng katika sehemu ya Kiungo Kinachoelekeza Kwingine.

Uonekanaji wa chaneli

Unaweza kuficha chaneli yako kwa muda kwa kuteua chaguo hili. Video, orodha na maelezo ya chaneli yako hayataonekana tena kwa watazamaji.

Kama mmiliki wa chaneli, bado unaweza kuona:

  • Ukurasa wa chaneli yako
  • Aikoni na sanaa ya chaneli yako
  • Video na orodha zako za video
  • Maoni na takwimu zako
  • Machapisho yako

Unaweza kufanya chaneli yako ionekane tena wakati wowote na maudhui yako yataonekana kwa umma na watazamaji.

Kumbuka: Uonekanaji wa chaneli unapatikana kwa washirika na watangazaji ambao msimamizi wao wa washirika au mwakilishi wao wa mauzo amewasha kipengele hiki.
Mafunzo kwa mifumo ya wengine

Unaweza kuteua chaguo hili ili uruhusu kampuni za wengine za AI zitumie maudhui yako ya YouTube kufunza mifumo ya AI wanayobuni.

Ili uwashe mipangilio ya mafunzo kwa mifumo ya wengine, teua Ruhusu kampuni za wengine zifunze mifumo ya AI kwa kutumia maudhui ya chaneli yangu katika Mipangilio ya Kina. Kisha, chagua kati ya:

  • Kampuni za wengine ulizochagua pekee: Hutoa ruhusa kwa kampuni unazochagua kwenye menyu kunjuzi pekee.
  • Kampuni zote za wengine: Hutoa ruhusa kwa kampuni zote za wengine.
Kumbuka: Mipangilio ya mafunzo kwa mifumo ya wengine inaweza kubadilishwa wakati wowote. Kunaweza kuwa na ucheleweshaji wa hadi siku 7 ili mabadiliko yaonekane katika kiolesura kinachoweza kufikiwa na umma (YouTube Data API). Pata maelezo zaidi kuhusu mafunzo kwa mifumo ya wengine.
Mipangilio mingine
Unaweza kudhibiti upatikanaji wa chaneli yako kwenye YouTube na kuondoa kabisa maudhui yako ukitumia mipangilio hii.

Kutimiza Masharti ya Kupata Vipengele

Kuangalia hali ya kutimiza masharti

Nufaika zaidi na maudhui yako ukitumia zana na vipengele vya ziada. Hapa, unaweza kuangalia ikiwa unatimiza masharti ya kupata vipengele vya kawaida, vya wastani au vya kina. Ili kuhakikisha jumuiya ya YouTube inakuwa salama kwa kila mtu, kupata vipengele vya wastani na vya kina kunahitaji hatua za ziada za uthibitishaji. Kuthibitisha utambulisho wako hutusaidia kupunguza matumizi mabaya na taka kwenye YouTube.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
3647650218232354674
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
false
true
true
true
true
true
59
false
false
false
false