Huenda ukaona ujumbe, "Chaneli yako ya YouTube ina maudhui lakini imezimwa" katika ukurasa wako wa Maudhui. Ukiona ujumbe huu, chaneli yako imefichwa na kwa sasa video na maudhui yako mengine hayawezi kutazamwa na wengine.
Huenda hali hii imetokea kwa sababu ulichagua kuficha chaneli yako kupitia mipangilio ya Akaunti ya Google.
Bado unaweza kutazama video, kupenda na kufuatilia na shughuli hizo zitafanyika kwa faragha kabisa. Ukitaka kufanya maudhui yako yaweze kutazamwa au kutumia vipengele vingine, lazima uwashe chaneli.
Jinsi ya kuwasha chaneli yako
- Ingia katika YouTube.
- Nenda kwenye fungua chaneli kisha ujaze fomu. Hatua hii itarejesha chaneli yako ya YouTube.
- Kwenye fomu, usibofye "Ili utumie jina la biashara au jina lingine, bofya hapa." Hatua hii itafungua chaneli badala ya kurejesha chaneli yako iliyofichwa.
Vidokezo:
- Baada ya kufungua upya chaneli yako ya umma, utaweza kufanya orodha na video zako ziweze kutazamwa kwenye ukurasa wa Video.
- Ukificha chaneli yako, huenda idadi ya mara za kutazamwa isiwe sahihi. Baada ya kufanya chaneli yako ionekane tena, inachukua hadi wiki moja kwa idadi ya mara za kutazamwa kusasishwa.
Ikiwa una Akaunti ya Biashara
- Ingia katika YouTube.
- Gusa picha yako ya wasifu
.
- Gusa Mipangilio
.
- Gusa Akaunti
Weka au udhibiti Chaneli zako.
- Chagua chaneli iliyofichwa.
- Ukiombwa ufungue chaneli, bofya Sawa.