Kuondoa maudhui yanayodaiwa kwenye video

Ikiwa video yako ina Dai la Content ID, huenda kukawa na vizuizi kuhusu pale ambapo video inaweza kutazamwa au iwapo inaweza kuchuma mapato. Ili uondoe dai na vizuizi husika, unaweza kuhariri na kuondoa maudhui yanayodaiwa bila kupakia video mpya.

Ukifanya hivyo, chaguo zozote kati ya hizi zitaondoa kiotomatiki dai la Content ID:

  • Punguza sehemu: Unaweza kuondoa tu sehemu inayodaiwa kwenye video yako.
  • Badilisha wimbo: Iwapo sauti katika video yako imedaiwa, unaweza kubadilisha sauti inayodaiwa na uweke sauti nyingine kutoka kwenye Maktaba ya Sauti katika YouTube.
  • Sitisha sauti ya wimbo: Iwapo sauti katika video yako imedaiwa, unaweza kusitisha sauti ambayo imedaiwa. Unaweza kuamua kuzima tu sauti ya wimbo au sauti ya video yote.

Kupunguza, kubadilisha au kuzima sauti ya maudhui yanayodaiwa kwenye Studio ya YouTube

Ili uondoe maudhui unayodai kwenye video:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui .
  3. Bofya upau wa kichujio kisha Hakimiliki.
  4. Tafuta video husika.
  5. Katika safu wima ya Vizuizi , wekelea kiashiria juu ya Hakimiliki.
  6. Bofya ANGALIA MAELEZO.
  7. Chini ya sehemu ya Maudhui yaliyotambuliwa katika video hii , tafuta dai husika na ubofye CHAGUA VITENDO kisha Punguza sehemu, Badilisha wimbo au Zima sauti ya wimbo.

 Kupunguza sehemu

Chaguo hili hukuruhusu kuhariri ili uondoe sehemu ya video yako iliyopata dai la Content ID.
  1. (Si lazima) Badilisha muda wa kuanza na muda wa kuisha wa sehemu unayoondoa.
    • Kumbuka kuwa ikiwa baadhi ya maudhui yaliyodaiwa yataendelea kuwepo kwenye video yako, dai halitaondolewa.
  2. Bofya ENDELEA kisha PUNGUZA.
Baada ya kuondoa maudhui yote yanaodaiwa, dai la Content ID litaondolewa kwenye video yako.

 Kubadilisha wimbo (madai ya sauti pekee)

Chaguo hili hukuruhusu kubadilisha sauti iliyodaiwa na sauti nyingine kutoka kwenye Maktaba ya Sauti ya YouTube.
  1.  Tumia vichujio vya utafutaji ili upate wimbo mpya wa sauti. Bofya Cheza ili uhakiki nyimbo.
  2. Unapopata wimbo unaopenda, bofya ONGEZA. Wimbo utaonekana kwenye kihariri katika kisanduku cha buluu.
    • Bofya na uburute kisanduku ili ubadilishe mahali pa wimbo kuanzia. Kumbuka kuwa iwapo baadhi ya sauti iliyodaiwa itaendelea kuwepo kwenye video yako, dai halitaondolewa.
    • Buruta kingo za kisanduku ili ubadilishe urefu wa wimbo.
    • Tumia chaguo za kukuza Zoom in ili urekebishe kwa usahihi zaidi.
  3. (Si lazima) Weka nyimbo zaidi.
  4. Bofya HIFADHI kisha BADILISHA.

Baada ya kubadilisha sauti yote inayodaiwa, dai la Content ID litaondolewa kwenye video yako.

 Kuzima sauti ya wimbo (madai ya sauti pekee)

Chaguo hili hukuruhusu kuzima sauti inayodaiwa katika video yako. Unaweza kuamua kuzima tu sauti ya wimbo au sauti ya video yote.
  1. Chagua jinsi ambavyo ungependa kuzima sauti:
    • Zima sauti yote wimbo unapocheza
      • Huzima sauti yote katika sehemu ya video yenye sauti inayodaiwa.
      • Chaguo hili kwa kawaida hufanya kazi haraka na linaweza kuondoa dai kiotomatiki.
    • Zima sauti ya wimbo tu (beta)
      • Huzima sauti ya wimbo unaodaiwa tu. Sauti nyingine, kama vile mazungumzo au madoido ya sauti, hazitazimwa.
      • Hatua hii kwa kawaida huchukua muda mrefu na huenda isifanye kazi iwapo wimbo hautaondolewa kwa urahisi.
  2. (Si lazima) Badilisha muda wa kuanza na muda wa kuisha kwa hatua ya kuzima sauti.
    • Kumbuka kuwa iwapo baadhi ya sauti inayodaiwa itaendelea kuwepo kwenye video yako, dai halitaondolewa.
  3. Angalia onyesho la kukagua la mabadiliko uliyofanya katika kicheza video.
  4. Bofya ENDELEA kisha ZIMA SAUTI. Mabadiliko yataanza kuchakatwa.

Iwapo sauti yote iliyodaiwa inaweza kuzimwa, dai la Content ID litaondolewa kwenye video yako.

Kumbuka:
  • Baada ya kufanya mabadiliko, muda wa kuchakata unaweza kutofautiana.
  • Huwezi kufanya mabadiliko mengine wakati video inachakata, lakini unaweza kufunga dirisha. Video itaendelea kuwa katika hali yake ya sasa (kabla ya mabadiliko) hadi uchakataji utakapokamilika.
  • Iwapo video yako ina urefu wa zaidi ya saa 6, huenda usiweze kuhifadhi mabadiliko.
  • Ikiwa kituo chako hakipo katika Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP), huenda usiweze kuhifadhi mabadiliko iwapo video yako imetazamwa zaidi ya mara 100,000.
Kidokezo: Uchakataji ukikamilika, pakia upya ukurasa ili uthibitishe mabadiliko yalifanywa na dai limeondolewa.

Kuzima maudhui yanayodaiwa kwenye programu ya Studio ya YouTube

Ili uzime maudhui yanayodaiwa kwenye video:

  1. Ingia katika akaunti kwenye programu ya Studio ya YouTube.
  2. Gusa Maudhui .
  3. Chagua video iliyo na kizuizi cha hakimiliki na uguse kizuizi.
  4. Katika kidirisha cha chini, gusa KAGUA MATATIZO.
  5. Gusa dai husika
  6. Gusa Zima sehemu.

Tendua mabadiliko

Ili utendue mabadiliko uliyofanya kwenye video yako na urejeshe video halisi:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui .
  3. Bofya kijipicha cha video unayotaka kubadilisha.
  4. Kwenye menyu ya kushoto, bofya Kihariri .
  5. Chagua Chaguo Morekisha Rejesha video halisi  ili uondoe mabadiliko yoyote uliyofanya kwenye video yako.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13238048399400799847
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false