Kuepuka vikwazo vya utiririshaji mubashara kwenye YouTube

Kabla ya kutiririsha mubashara kwenye kifaa cha mkononi, unahitaji kutimiza masharti yetu ya kutiririsha maudhui mubashara kwenye vifaa vya mkononi.

Uwezo wa kituo chako kutiririsha maudhui mubashara unaweza kuzimwa kabisa au kwa muda kutokana na sababu mbalimbali. Ikiwa akaunti yako imezuiwa isitiririshe mubashara, huruhusiwi kutumia kituo kingine kutiririsha mubashara kwenye YouTube. Kikwazo hiki kinatumika tu mradi masharti yanaendelea kutumika kwenye akaunti yako. Ukiukaji wa vikwazo hivi unachukuliwa kuwa ukwepaji kwa mujibu wa Sheria na Masharti yetu na huenda ukasababisha kufungwa kwa akaunti yako.

Soma hapa chini ili uone orodha ya sababu ambazo zimepelekea uwezo wa kituo chako kutiririsha maudhui mubashara kuzimwa kabisa au kwa muda:

Vikwazo vya Mwongozo wa Jumuiya

  • Kituo chako kimepokea onyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya au mtiririko mubashara umeondolewa kwa mujibu wa sera zetu.

  • Mtiririko wako mubashara unalingana na matangazo mengine ya moja kwa moja yaliyo na hakimiliki.
  • Mtiririko wako mubashara unawaangazia watoto. Ili kulinda watoto ipasavyo kwenye YouTube, haturuhusu watoto walio na umri wa chini ya miaka 13 kutiririsha mubashara isipokuwa waandamane na mtu mzima. Vituo ambavyo havitii sera hii vinaweza kupoteza kabisa au kwa muda mfupi uwezo wa kutiririsha mubashara. 
  • Kwa vituo vilivyo na idadi kubwa ya video zenye vipengele vilivyozimwa, uwezo wa kutiririsha mubashara unaweza pia kuzimwa. Angalia ikiwa kituo chako kina maonyo yoyote na endapo una idhini ya kutiririsha mubashara kwa sasa.
  • Ukipendekeza kuwa utatiririsha mubashara maudhui yanayokiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya, huenda tukayawekea maudhui hayo mipaka ya umri, kuyaondoa au kuzima uwezo wa kituo chako kutiririsha mubashara. 
  • Haturuhusu mitiririko mubashara inayoonyesha mtu akiwa amebeba, kushika au kusafirisha bunduki. Mtiririko mubashara unaokiuka sera ya YouTube ya kudhibiti bunduki utaondolewa kwenye vituo ambavyo havitii sera, pia kituo kinaweza kupoteza kabisa au kwa muda uwezo wa kutiririsha mubashara.

Vikwazo vya hakimiliki

  • Mtiririko wako mubashara unaoendelea au uliowekwa kwenye kumbukumbu umepata onyo la hakimiliki.
  • Mtiririko wako mubashara unalingana na matangazo mengine ya moja kwa moja yaliyo na hakimiliki.

Vikwazo vya “Maudhui yanayolenga watoto”

Ikiwa kituo chako au hadhira ya mtiririko wako mubashara imebainishwa kuwa inalenga watoto, baadhi ya vipengele vitazimwa au kudhibitiwa. Pata orodha kamili ya vipengele vilivyoathiriwa na mipangilio ya hadhira "inayolenga watoto"..

Soma hapo chini ili kuona mifano michache:

Vipengele vilivyozimwa

  • Gumzo la moja kwa moja: Gumzo la moja kwa moja, kipengele cha kuonyesha tena gumzo la moja kwa moja na Super Chat.
  • Maoni: Maoni kwenye kumbukumbu za mtiririko mubashara na mitiririko ijayo.
  • Arifa za vikumbusho: Arifa za vikumbusho vya mitiririko ijayo.

Vipengele vilivyowekewa vikwazo

  • Kuangazia video: Kipengele cha kuangazia video zilizotayarishwa kutoka kwenye seti ya video asili kama zinazolenga watoto zitakuwa na vikwazo sawa na vya asili.
  • Matangazo: Matangazo yaliyowekewa mapendeleo yatazimwa kwenye mitiririko mubashara na Maonyesho ya kwanza. Matangazo yenye muktadha yanaweza kuonyeshwa.

Vikwazo vingine

Ikiwa umefikisha kikomo chako cha kila siku cha kutayarisha mitiririko mubashara, unaweza kujaribu tena baada ya saa 24.

Matangazo

Kumbuka - Mwongozo na vikwazo vya Maudhui Yanayofaa Watangazaji kuhusu Kulipia bidhaa zitangazwe katika maudhui na maudhui yaliyoidhinishwa yanatumika pia kwenye mitiririko mubashara.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5591601464810631927
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false