Kuwasilisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki

Iwapo maudhui yako yanayolindwa na hakimiliki yamechapishwa kwenye YouTube bila idhini yako, unaweza kuwasilisha ombi la kuondolewa kwa maudhui hayo kwa kukiuka hakimiliki. Kuwasilisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki ni mchakato wa kisheria.

Kutayarisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki

Kabla ya kuwasilisha ombi la kuondolewa kwa video kwa kukiuka hakimiliki, unahitaji kuzingatia yafuatayo:

  1. Hali zisizofuata kanuni za hakimiliki: Zingatia iwapo kanuni ya matumizi ya haki, matumizi yasiyo ya biashara au hali sawa isiyofuata kanuni za hakimiliki inatumika. Tunaweza kukuomba uthibitishe kuwa umezingatia haya. Hatutaondoa maudhui ambayo umebainisha kwenye ombi lako la kuondoa maudhui ikiwa hutajibu ipasavyo au ikiwa yanafuata kanuni za hali zisizofuata kanuni za hakimiliki.
  2. Taarifa binafsi: Hakikisha unaelewa jinsi maelezo yako ya mawasiliano yanavyotumika ukishatuma ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki.
  • Kumbuka kuwa ombi hili la kuondoa maudhui linapaswa kuwasilishwa na mwenye hakimiliki au mwakilishi rasmi aliyeidhinishwa kuchukua hatua kwa niaba ya mmiliki.

Maombi yaliyoratibiwa ya kuondoa maudhui: Zingatia kuratibu ombi lako la kuondoa maudhui ili litekelezwe ndani ya siku 7. Hatua hii inampa aliyepakia siku 7 za kufuta maudhui ili aepuke chaneli yake kupewa onyo la hakimiliki.

Kuwasilisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki

Njia ya haraka na rahisi zaidi ya kuwasilisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki ni kujaza fomu yetu ya wavuti kwenye kompyuta. Unaweza pia kuwasilisha maombi ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki kupitia barua pepe, faksi na barua.

Usiwasilishe madai ya uongo. Matumizi mabaya ya fomu ya wavuti ya kuwasilisha ombi la kuondoa video, kama vile kutoa taarifa za uongo, yanaweza kufanya akaunti yako isimamishwe au huenda ukachukuliwa hatua za kisheria.

Bofya kitufe hiki ili ufungue fomu ya wavuti:

Wasilisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki

Unaweza pia kufikia fomu hii ya wavuti moja kwa moja kwenye Studio ya YouTube:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Hakimiliki .
  3. Bofya OMBI JIPYA LA KUONDOA VIDEO.

 

Maudhui yasiyo ya video: Huwezi kutumia fomu yetu ya wavuti kutuma maombi ya kuondolewa kwa maudhui yasiyo video, kama vile picha za bango la chaneli. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuwasilisha ombi la kuondoa maudhui yasiyo video.

Kuzuia upakiaji upya

Kwenye fomu ya wavuti, unaweza kuteua chaguo la kuzuia nakala za video unazoripoti kupakiwa tena kwenye YouTube. Ukiteua chaguo hili, anwani yako ya barua pepe na jina la mwenye hakimiliki huenda zikaonyeshwa kwa aliyepakia video ambazo zimezuiwa kupakiwa upya. Pata maelezo kuhusu kuzuia upakiaji tena wa video zilizoondolewa.

Kudhibiti maombi yako ya kuondoa video

Ili uangalie maombi ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki ambayo uliwasilisha awali kwenye YouTube:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, bofya Hakimiliki .
  3. Bofya Maombi ya Kuondoa Video.

Ikiwa unadhibiti maudhui mengi yaliyo na hakimiliki na mara nyingi unahitaji kutuma maombi ya kuondoa maudhui, unaweza kuwa umetimiza masharti ya kutumia zana za kina zaidi za udhibiti wa hakimiliki. Pata maelezo zaidi kuhusu Zana za YouTube za kudhibiti hakimiliki.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu maombi ya kuondoa video, ikiwa ni pamoja na kile kinachotokea baada ya kuwasilisha ombi la kuondoa, nenda kwenye muhtasari wetu wa mchakato wa ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11277364826778456541
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false