Vidokezo vya kuunda faili ya unukuzi

Faili za unukuzi ni njia rahisi ya kutayarisha manukuu. Zina maandishi ya kilichosemwa kwenye video na zinaweza kuwa na sura za video. Unaweza kuweka faili ya unukuzi moja kwa moja kwenye video yako au ufuate hatua zilizo hapo chini ili utayarishe faili ya unukuzi.

Faili za unukuzi hufanya kazi vizuri zaidi kwenye video ambazo zina urefu usiozidi saa moja ambazo zina ubora wa juu wa sauti na matamshi dhahiri. Faili ya unukuzi inapaswa kuwa katika lugha sawa na mazungumzo yaliyo kwenye video. Baada ya kuunda faili, fuata maagizo ya kuipakia kwenye video yako.

Kuweka muundo wa faili yako ya unukuzi

Andika maandishi ya kilichosemwa kwenye video yako kisha uyahifadhi kama faili ya maandishi dhahiri (.txt). Unaweza kugeuza miundo mingine (kama vile Microsoft Word, HTML) iwe faili ya maandishi dhahiri au unaweza kutumia programu za mfumo kwenye kompyuta yako kama vile Notepad.

Ili upate matokeo bora zaidi, tumia vidokezo hivi vya muundo:

  • Ili ulazimishe mwanzo wa manukuu mapya, tumia mstari tupu.
  • Ili ubainishe sauti za chinichini, tumia mabano mraba. Kwa mfano, [muziki] au [kicheko].
  • Weka >> kutambua wanaozungumza au mabadiliko ya mzungumzaji.

Ufuatao ni mfano wa jinsi faili yako ya unukuzi inavyoweza kuonekana:

>> Fatuma: Hujambo, jina langu ni Fatuma Abdi na huyu ni Juma Hassan

>> Juma: na sisi ndio wamiliki wa Tanuri Mikate ya Abdi.

>> Fatuma: Leo tutawafundisha jinsi ya kutengeneza
biskuti zetu maarufu zenye vipande vya chokoleti!

[muziki wa utangulizi]

Sawa, kwa hivyo tayari tuna viungo vyote hapa

Kuhifadhi faili zisizo za Kiingereza

Kwa faili za unukuzi zisizo za lugha ya Kiingereza, tunapendekeza uhifadhi faili kwa kutumia usimbaji wa UTF-8 ili kuboresha usahihi wa onyesho:

Maagizo ya kompyuta binafsi
  1. Fungua Notepad.
  2. Bofya Faili kisha Hifadhi kama.
  3. Chagua UTF-8 kwenye sehemu ya “Usimbaji.”
Maagizo ya kompyuta ya Apple
  1. Fungua TextEdit.
  2. Bofya Muundo, kisha uchague Unda Maandishi Dhahiri.
  3. Bofya Faili, kisha Hifadhi.
  4. Chagua Unicode (UTF-8).

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14477828432693566334
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false