Kubadilisha au kuondoa manukuu

Badilisha manukuu

Unaweza kubadilisha maandishi na mihuri ya wakati ya manukuu yako. Unaweza pia kutumia huduma au programu za kuhariri manukuu.

Hariri maandishi ya manukuu

Kumbuka: Ikiwa unahariri manukuu yaliyotungwa kiotomatiki, kikundi kipya cha manukuu kinachojumuisha mabadiliko yako kitazalishwa.

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Manukuu.
  3. Bofya video ambayo ungependa kuhariri.
  4. Kwa lugha ambayo ungependa kuhariri, katika safu wima ya “Manukuu” chagua Badilisha.
  5. Kwa manukuu ya kiotomatiki, chagua TOA NAKALA NA BADILISHA kisha ENDELEA ili ubatilishe rasimu iliyopo. 
  6. Bofya ndani ya mstari wowote katika kidirisha cha kikundi cha manukuu na ubadilishe maandishi.
  7. Ukishamaliza kufanya mabadiliko, bofya Chapisha.
Badilisha muda wa manukuu

Unaweza kubadilisha saa ya vikundi vya manukuu yako moja kwa moja kwenye kihariri cha manukuu cha YouTube au kwa kupakua faili za manukuu yako.

Kutumia kihariri cha manukuu cha YouTube

  1. Ingia katika akaunti kwenye Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Manukuu.
  3. Bofya video ambayo ungependa kuhariri.
  4. Kwa lugha ambayo ungependa kuhariri, katika safu wima ya “Manukuu”,  chagua Badilisha.
  5. Chagua mstari mahususi katika kidirisha cha kikundi cha manukuu:
    1. Unaweza kurekebisha muda kwa kubadilisha vidirisha viwili vya muhuri wa wakati kando ya kikundi cha manukuu.
  6. Ukishamaliza kufanya mabadiliko, bofya Chapisha.

Pakua na ubadilishe faili za manukuu

Unaweza kubadilisha mihuri ya wakati kwa kupakua faili ya manukuu na kutumia programu ya kuhariri maandishi dhahiri (.txt) kama vile TextEdit au Notepad ili kufanya mabadiliko. 

  1. Ingia katika akaunti kwenye Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Manukuu.
  3. Bofya video ambayo ungependa kuhariri.
  4. Chini ya Manukuu, bofya BADILISHA kando ya lugha unayotaka kubadilisha.
  5. Bofya Chaguo '' na uchague Pakua manukuu. Pata maelezo zaidi kuhusu aina ya faili za manukuu
  6. Kivinjari chako kitapakua faili iliyo na kikundi cha manukuu. Badilisha faili na uihifadhi.
  7. Fuata maagizo ya kupakia manukuu kwenye video yako tena.

Kuondoa manukuu

Ili usimamishe manukuu yasionyeshwe kwenye video yako, unaweza kuyafuta kabisa kwenye video yako na Akaunti ya Google.

  1. Ingia katika akaunti kwenye Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Manukuu.
  3. Kwa lugha ambayo ungependa kufuta,  katika safu wima ya “Manukuu”,  teua Chaguo '' kisha Futa .
  4. Utaombwa uthibitishe kuwa unataka kufuta manukuu. Bofya FUTA MANUKUU.

Kumbuka: Baada ya kufuta manukuu ya kiotomatiki kwenye video, huwezi kuyawasha tena.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8719545180898959407
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false