Faili za manukuu zinazoweza kutumika

Faili ya manukuu ina maandishi ya mambo yanayosemwa kwenye video. Pia inaonyesha muda ambapo kila mstari wa maandishi unapaswa kuonyeshwa. Baadhi ya faili pia zina maelezo ya nafasi na muundo, ambayo ni muhimu kwa watazamaji viziwi au walio na matatizo ya kusikia. Angalia aina za faili zinazoweza kutumika kwenye YouTube hapo chini.

Ni mara yako ya kwanza? Jaribu kuweka manukuu moja kwa moja kwenye video yako kwa kutumia kihariri chetu cha manukuu.
Aina za msingi za faili

Ikiwa ni mara yako ya kwanza kuunda faili za manukuu, tunapendekeza utumie mojawapo ya aina zifuatazo za faili:

Jina la muundo Kiambishi cha faili Maelezo zaidi
SubRip .srt Unaweza tu kutumia matoleo ya msingi ya faili hizi. Maelezo ya muundo (lebo) hayatambuliwi. Ni lazima faili iwe katika maandishi dhahiri ya UTF-8.
SubViewer .sbv au .sub Unaweza tu kutumia matoleo ya msingi ya faili hizi. Maelezo ya muundo (lebo) hayatambuliwi. Ni lazima faili iwe katika maandishi dhahiri ya UTF-8.
MPsub (manukuu ya MPlayer) .mpsub Kigezo cha "FORMAT=" kinaweza kutumika.
LRC .lrc Maelezo ya muundo (lebo) hayatambuliwi, lakini muundo ulioboreshwa unaweza kutumika.
Videotron Lambda .cap Kimsingi, aina hii ya faili hutumiwa kwenye manukuu ya Kijapani.
 

Ikiwa ni mara yako ya kwanza kuunda faili za manukuu, huenda ukahitaji kutumia SubRip (.srt) au SubViewer (.sbv). Miundo hiyo inahitaji tu maelezo ya msingi ya muda na unaweza kuihariri kwa kutumia programu yoyote ya kuhariri maandishi dhahiri.

Tofauti kuu kati ya faili za SubRip na SubViewer ni muundo wa wakati wa kuanza na kukamilika kwa manukuu. Ifuatayo ni mifano ya miundo yote miwili:

Mfano wa SubRip (.srt)
1
00:00:00,599 --> 00:00:04,160
>> Fatuma: Hujambo, jina langu ni Fatuma Abdi na huyu ni Juma Hassan

2
00:00:04,160 --> 00:00:06,770
>> Juma: na sisi ndio wamiliki wa Tanuri Mikate ya Abdi.

3
00:00:06,770 --> 00:00:10,880
>> Fatuma: Leo tutawafundisha jinsi ya kutengeneza
biskuti zetu maarufu zenye vipande vya chokoleti!

4
00:00:10,880 --> 00:00:16,700
[muziki wa utangulizi]

5
00:00:16,700 --> 00:00:21,480
Sawa, kwa hivyo tayari tuna viungo vyote hapa
Mfano wa SubViewer (.sbv)
0:00:00.599,0:00:04.160
>> Fatuma: Hujambo, jina langu ni Fatuma Abdi na huyu ni Juma Hassan

0:00:04.160,0:00:06.770
>> Juma: na sisi ndio wamiliki wa Tanuri Mikate ya Abdi.

0:00:06.770,0:00:10.880
>> Fatuma: Leo tutawafundisha jinsi ya kutengeneza
biskuti zetu maarufu zenye vipande vya chokoleti!

0:00:10.880,0:00:16.700
[muziki wa utangulizi]

0:00:16.700,0:00:21.480
Sawa, kwa hivyo tayari tuna viungo vyote hapa
Aina za kina za faili

Tumia aina hizi za faili ikiwa ungependa kuwa na udhibiti zaidi wa muundo (lebo) au nafasi ya kuweka manukuu yako.

Jina la muundo Kiambishi cha faili Maelezo zaidi
SAMI (Synchronized Accessible Media Interchange) .smi au .sami Mihuri ya wakati, maandishi na lebo rahisi pekee (<b>, <i>, <u> na
color= attribute within a <font>) zinaweza kutumika. Huwezi kuweka nafasi ya manukuu.
RealText .rt Mihuri ya wakati, maandishi na lebo rahisi pekee (<b>, <i>, <u> na
color= attribute within a <font>) zinaweza kutumika. Huwezi kuweka nafasi ya manukuu.
WebVTT .vtt Katika utekelezaji wa kwanza. Unaweza kuweka nafasi ya manukuu, lakini unaweza tu kutumia muundo wa <b>, <i>, <u> kwa sababu majina ya aina za vipengee vya CSS bado hayajasawazishwa.
TTML (Timed-Text Markup Language) .ttml Katika utekelezaji usio kamili. Viendelezi vya SMPTE-TT vinaweza kutumika kwenye vipengele vya CEA-608. Unaweza kutumia aina ya faili ya iTunes Timed Text (iTT); iTT ni sehemu ya TTML, Toleo la 1.0. Unaweza kubainisha muundo na nafasi ya
manukuu.
DFXP (Distribution Format Exchange Profile) .ttml au .dfxp Aina hizi za faili hufasiriwa kama faili za TTML. 
Aina za faili za vituo vya utangazaji (televisheni na filamu)

Kwa kawaida aina hizi za faili hutumiwa kwenye manukuu ya maudhui ya utangazaji (televisheni na filamu) na zinaruhusu viwango vya CEA-608 au EBU-STL. YouTube hujaribu kuonyesha manukuu kutoka kwenye faili hizi kana kwamba yako kwenye runinga — kwa kutumia muundo, rangi na nafasi sawa.

Jina la muundo Kiambishi cha faili Maelezo zaidi
Manukuu ya Scenarist .scc Faili hizi zina uwakilishaji halisi wa data ya CEA-608, ambao ndio muundo unaopendelewa wakati manukuu yanategemea vipengele vya CEA-608.
EBU-STL (mfumo wa jozi) .stl Kiwango cha Shirika la Utangazaji la Ulaya.
Caption Center (mfumo wa jozi) .tds Inaruhusu vipengele vya CEA-608.
Captions Inc. (mfumo wa jozi) .cin Inaruhusu vipengele vya CEA-608.
Cheetah (maandishi ya ASCII) .asc Inaruhusu vipengele vya CEA-608.
Cheetah (mfumo wa jozi) .cap Inaruhusu vipengele vya CEA-608.
NCI (mfumo wa jozi) .cap Inaruhusu vipengele vya CEA-608.
 
Tunapendelea aina ya faili za Manukuu ya Scenarist (kiambishi cha faili cha .scc). Faili hizi zina uwakilishaji halisi wa data ya CEA-608, ambao ndio muundo unaopendelewa wakati manukuu yanategemea vipengele vya CEA-608.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14203843496586592100
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false