Kununua au kukodi filamu na vipindi vya televisheni kwenye YouTube

Kulingana na mahali ulipo, unaweza kununua au kukodi filamu mahususi kwenye YouTube. Chagua miongoni mwa maelfu ya filamu zilizoshinda tuzo, filamu bora za zamani na filamu mpya.

Ikiwa uko nchini Marekani, Ujerumani, Ufaransa, Australia au Uingereza, unaweza pia kujisajili kwenye baadhi ya Vituo vya Primetime, kama vile Showtime au Starz. Kujisajili kwenye chaneli hizi hukuwezesha utazame vipindi kwenye YouTube bila kuhitaji kubadilisha kati ya programu na huduma tofauti za kutiririsha.

Kumbuka: Filamu ulizonunua kwenye YouTube hazitaonekana kwenye Maktaba yako ya Familia ya Google Play. Pata maelezo zaidi.

Pata maelezo kuhusu mahali unapoweza kununua na kukodi filamu kwenye YouTube

Kununua au kukodi filamu katika maeneo haya

  • Ajentina
  • Australia
  • Austria
  • Ubelgiji
  • Bosnia na Hezegovina
  • Brazili
  • Kanada
  • Kuprosi
  • Zechia
  • Denmaki
  • Ufini
  • Ufaransa
  • Ujerumani
  • Ugiriki
  • Hong Kong
  • Hangaria
  • India
  • Indonesia
  • Ayalandi
  • Italia
  • Japani
  • Lativia
  • Litwania
  • Malta
  • Meksiko
  • Masedonia Kaskazini
  • Uholanzi
  • Nyuzilandi
  • Norwe
  • Ufilipino
  • Polandi
  • Ureno
  • Urusi
  • Senegali
  • Singapoo
  • Slovakia
  • Slovenia
  • Korea Kusini
  • Uhispania
  • Uswidi
  • Uswizi
  • Taiwani
  • Uganda
  • Ukraini
  • Uingereza
  • Marekani

Kununua vipindi vya televisheni katika maeneo haya

Nunua kila kipindi kivyake au misimu mizima. Ukinunua msimu ambao haujatolewa kabisa, vipindi vitaongezwa kiotomatiki kwenye maktaba yako baada ya kutolewa.
  • Australia
  • Kanada
  • Ufaransa
  • Ujerumani
  • Japani
    • Kumbuka: Unaweza pia kukodi vipindi vya televisheni nchini Japani. Chaguo hili halipatikani kwa sasa katika nchi na maeneo mengine yoyote.
  • Uswizi
  • Uingereza
  • Marekani

Pata maelezo kuhusu mahali unapoweza kununua na kukodi filamu kwenye YouTube

  • Sharti uwe na umri wa miaka 18 au zaidi ili uweze kununua au kukodi.
  • Unaweza kununua au kukodi filamu na vipindi vya televisheni kwenye vifaa fulani pekee. 
  • Upatikanaji wa filamu mahususi hutofautiana kulingana na eneo na huenda ukabadilika kadri muda unavyosonga.
  • Utahitaji muunganisho wa intaneti ili utazame maudhui uliyoyakodi au kununua. 
  • Baada ya kukodi filamu, una siku 30 za kuanza kuitazama. Baada ya kuanza kutazama filamu, unaweza kuitazama mara nyingine upendavyo hadi kipindi chako cha kukodi kiishe. Kwa kawaida vipindi vya ukodishaji huwa saa 48 lakini ukurasa wa mwisho wa malipo ya ukodishaji utabainisha urefu wa kipindi chako cha kukodi.
  • Kwa baadhi ya video, bei tofauti za viwango mbalimbali vya ubora zinaweza pia kupatikana. Uchezaji wa filamu za HD na UHD unapatikana tu kwenye vifaa fulani vinavyotumika na kwa kasi fulani za intaneti. Angalia masharti ya vifaa vya HD/UHD ili upate maelezo zaidi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
16841466329628934814
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false