Kukubali mwaliko wa akaunti ya Kidhibiti Maudhui

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika ambao hutumia Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube. Wasiliana na Msimamizi wako wa Washirika wa YouTube ili uweze kuvitumia.

Unapopata mwaliko wa kujiunga kwenye akaunti ya shirika lako ya Kidhibiti Maudhui, unahitaji kukubali mwaliko kabla upate idhini ya kufikia Kidhibiti Maudhui.

Jinsi ya kukubali mwaliko

  1. Fungua barua pepe ya mwaliko. Barua pepe imetumwa kutoka noreply@youtube.com na ina mada ya Mwaliko wa kudhibiti maudhui ya {your organization} kwenye YouTube.

  2. Bofya kiungo kilicho katika sehemu ya ujumbe wa barua pepe.
  3. Ingia katika akaunti ya YouTube ukitumia akaunti ya Google unayotaka kutumia kudhibiti maudhui ya shirika lako. Unaweza kutumia akaunti iliyopo ya Google au ufungue akaunti ya Google.
    • Chagua Tumia akaunti iliyopo ya Google ikiwa una akaunti iliyopo ya Google unayotumia kwenye kazi.
    • Chagua Fungua akaunti mpya ya Google ikiwa huna akaunti ya Google au ungependa kufungua akaunti tofauti ya kudhibiti maudhui ya shirika lako.

Baada ya kuingia katika akaunti, unaweza kuanza kudhibiti maudhui ya shirika lako, kulingana na ruhusa ulizopewa na mtu aliyekualika.

Pata maelezo zaidi kuhusu vipengele na zana za Kidhibiti Maudhui: Fahamu jinsi ya kutumia Kidhibiti Maudhui cha Studio.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14329088793298407255
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false