Kubadilisha usambazaji wa video

Mipangilio ya usambazaji inakuwezesha kuchagua ikiwa ungependa video zako zipatikane kwenye mifumo yote, au mifumo ya kuchumia mapato pekee. Watumiaji ambao si washirika wa kuchuma mapato hawawezi kubadilisha mipangilio ya usambazaji.

Weka mipangilio ya usambazaji wa video

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye Menyu ya kushoto, chagua maudhui kisha video ambayo ungependa kuhariri.
  3. Sogeza hadi mwisho wa menyu kisha bofya ONYESHA ZAIDI.
  4. Kwenye sehemu ya "Leseni na usambazaji" katika kisanduku cha Usambazaji, chagua “Kila mahali” au “Video hii ipatikane kwenye mifumo ya kuchumia mapato pekee”.
  5. Chagua Hifadhi.

Video zenye madai

Mipangilio ya usambazaji inayotumika kwenye video inategemea ikiwa video ina maudhui yanayodaiwa.

  • Ikiwa video ni video inayodaiwa, mipangilio ya usambazaji ya mlalamishi, si mtumiaji, itatumika.
  • Iwapo muziki unaochezwa kwenye video unadaiwa, mipangilio ya usambazaji ya mlalamishi, si mtayarishi, itatumika kwa video hiyo.

Tofauti kati ya mifumo ya kuchumia mapato na mifumo yote

Ifuatayo ni mifumo inayochukuliwa kuwa ya kuchumia mapato:

  • www.youtube.com
  • Programu ya YouTube
  • Programu ya YouTube kwenye TV pamoja na kwenye Xbox, Android TV, PlayStation na Chromecast
  • Unaweza kufikia m.youtube.com kwenye simu nyingi mahiri
  • Programu ya YouTube kwenye Apple TV

Kando na mifumo ya kuchumia mapato iliyotajwa hapa juu, "mifumo yote" inajumuisha, lakini si tu, yafuatayo:

  • Programu ya YouTube iliyosakinishwa kwenye iOS 5 na matoleo ya awali
  • Matoleo ya zamani ya programu za YouTube kwenye TV au simu za msingi
  • m.youtube.com inaweza kufikiwa kwenye simu za msingi

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
12760734551828951250
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false