Kutumia YouTube iliyo na kisoma skrini

Furahia hali bora zaidi ya utumiaji wa YouTube iliyo na kisoma skrini cha kompyuta ukitumia vidokezo kwenye ukurasa huu. Mikato ya kibodi huwashwa kiotomatiki unapotumia YouTube.

Kutafuta kwenye YouTube na Matokeo ya utafutaji

Kutafuta video za YouTube

  1. Nenda kwenye YouTube.
  2. Nenda kwenye kisanduku cha Kutafutia katika sehemu ya juu ya ukurasa ukitumia / kitufe cha kibodi. 
  3. Weka hoja ya utafutaji kisha kisha ubonyeze Enter.

Matokeo ya utafutaji

Ukurasa wa matokeo ya utafutaji una sehemu ya "Je, ulimaanisha" ambayo inapendekeza maneno sahihi ikiwa ulikosea tahajia yoyote. Kila moja ya matokeo ya utafutaji lina maelezo yafuatayo:

  • Jina la video  -- Ukilichagua itacheza video. 
  • Jina la chaneli iliyochapisha video.
  • Video ina muda kiasi gani tangu ilipopakiwa na imetazamwa mara ngapi.
  • Kijisehemu kutoka kwenye maelezo ya video.

Kichezaji cha YouTube

Unapobofya video, utaenda kwenye kicheza video za YouTube. Zifuatazo ni sehemu za kichezaji utakazotumia hapa:

Vichwa vya sehemu

H1 kwenye kichwa cha video

Kwenye kichezaji

  • Kitelezi cha kusogeza: Kitelezi cha kusogeza hutumika kusogeza mbele haraka au kurudisha nyuma video. Ili utumie kitelezi cha kusogeza, zima kwanza Kiteuzi pepe kisha kichupo kwenye kitelezi. Tumia vishale vya kushoto au kulia au vya juu au chini ili upeleke mbele au kurudisha nyuma video kwa haraka.
  • Cheza au sitisha: Kitufe cha maandishi hubadilika kulingana na hali ya video. Ili ucheze video, chagua kitufe cha Kucheza au kitufe cha K baada ya video kuacha kucheza.
  • Inayofuata: Kitufe hiki hukuruhusu uruke ili uende kwenye video inayofuata. Ikiwa huna vitufe vya maudhui, unaweza kuruka ili uende kwenye video inayofuata ukitumia Shift pamoja na N
  • Kuzima au kurejesha sauti: Kitufe hiki hubadilika kulingana na iwapo video imezimwa sauti au la.
  • Kitelezi cha sauti: Tumia vishale vya kushoto au kulia au vya juu au chini ili uongeze au upunguze sauti.
  • Muda uliopita au jumla ya muda: sehemu hii inaonyesha jumla ya muda uliopita katika jumla ya muda wa video. Inakuonyesha ni kiasi gani cha video ambacho tayari kimecheza na ni kiasi gani bado kinasalia kucheza. 
  • CC (Manukuu): Ikiwa video ina manukuu, unaweza kuyawasha kupitia njia ya mkato ya C. Manukuu yatakuwa katika sehemu ya chini ya video. Ili uzime manukuu, tumia njia ya mkato ya C tena.

Mipangilio 

Kitufe hiki cha Mipangilio hufungua menyu inayokuruhusu ufanye mabadiliko yafuatayo:

  • Vidokezo: Washa au uzime vidokezo.
  • Kasi ya kucheza: Chagua kasi ya kucheza ya video kutoka kwa ya kawaida, ongeza kazi au punguza kasi.
  • Manukuu: Washa au zima manukuu. Unaweza pia kuchagua lugha ya manukuu hapa, au uchague tafsiri ya kiotomatiki.
  • Ubora: Chagua ubora wa pikseli wa video unayotazama sasa hivi. Ubora unaopatikana unategemea jinsi video ilivyopakiwa na kasi ya intaneti yako. Tunapendekeza uache chaguo hili kwenye hali ya Kiotomatiki ili ubora wa video uchaguliwe kulingana na kasi ya intaneti yako.

Hali ya ukumbi wa filamu

Chagua Hali ya ukumbi wa filamu  ili kupanua kichezaji. Ili kurudi kwenye ukubwa halisi wa kichezaji, iteue tena.

Skrini nzima

Kuchagua skrini nzima  huongeza kichezaji kwa ukubwa wa skrini yako na kuondoa kila kitu nje ya kichezaji. Ili uondoke katika hali ya skrini nzima, chagua Escape.

Skrini nzima hutumika pia unapotaka kuondoa vipengele vya ziada katika ukurasa wa HTML vinavyozunguka kichezaji. Hali hii itaacha kichezaji peke yake.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13311793650386789107
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false