Makala haya ni ya watayarishi walio katika Mpango wa Washirika wa YouTube (ikiwa ni pamoja na washirika wa Mtandao wa Chaneli Mbalimbali) ambao wangependa kubadilisha aina za matangazo yanayoonyeshwa katika maudhui yao.
Ikiwa wewe ni mtazamaji, soma makala haya ili upate maelezo zaidi kuhusu matangazo kwenye video unazotazama.Mabadiliko ya hivi majuzi kwenye aina nyeti za matangazo:
- Tarehe 15 Mei, 2025, aina nyeti ya “Michezo ya Video (ya Kawaida na ya Mtandaoni)” itaondolewa kwenye Aina za matangazo katika Studio ya YouTube. Wanaotumia mipangilio hii kwa sasa wana hadi tarehe 15 Juni, 2025 kabla ya vizuizi vilivyopo kuacha kutumika. Uwezo wa kuzuia matangazo ya michezo ya video sasa utapatikana tu kwenye:
- Aina za jumla: Mapendeleo, Michezo na Burudani > Michezo na Vifaa vya Watoto Kuchezea > Michezo.
- Katika sehemu ya Michezo: Zuia matangazo ya michezo ya video kwenye Mafumbo na Michezo ya Mtandaoni na/au Michezo ya Video, Vifuasi na Vifaa vya Michezo ya Video pamoja na aina zozote ndogo.
- Tarehe 15 Julai, 2025, aina nyeti ya “Ngozi Isiyofunikwa Kwa Mavazi (Picha Pekee)” pia itaondolewa. Wanaotumia mipangilio hii kwa sasa wana hadi tarehe 15 Agosti, 2025 kabla ya vizuizi vilivyopo kuacha kutumika.
Tunapendekeza utumie mojawapo ya aina zifuatazo badala yake:
- Aina nyeti: Inataja Ngono
- Aina za jumla: Mavazi > Mavazi > Mavazi ya ndani au Mavazi ya kuogelea
Huenda hungependa kuona matangazo fulani karibu au kwenye video au chaneli yako ya YouTube kutokana na imani binafsi, sababu za kibiashara au za maudhui. Ukiwa mtayarishi, unaweza kuzuia matangazo fulani yasionekane karibu au kwenye maudhui na chaneli yako ya YouTube, ukitumia vidhibiti vya kuzuia matangazo katika Studio ya YouTube.
Kuzuia matangazo kunaweza kuwa na athari mbaya katika mapato yako, kwa hivyo ni muhimu kuchagua kidhibiti kinachosawazisha malengo yako ya kuchuma mapato na sababu zako za kuzuia. Tunapendekeza uanze na kidhiti kinachozuia matangazo machache kwanza, kama vile kuzuia URL mahususi.
Vidhibiti vya kuzuia matangazo vinayvopatikana
URL mahususi
Unaweza kuzuia matangazo yanayoelekeza kwenye URL mahususi. Hii inaweza kukufaa ikiwa hungependa kuona matangazo yanayoelekeza kwenye tovuti mahususi.
Unaweza kuzuia hadi URL 500. Ikiwa umefikia kikomo na unahitaji kuzuia URL mpya, utahitaji kuondoa kizuizi kwenye URL uliyozuia kwanza.
Aina za jumla
Unaweza kuzuia matangazo kutoka kwenye aina za jumla, kama vile Mavazi, Bunduki au Magari. Hii inaweza kukufaa ikiwa ungependa kuzuia matangazo yanayohusiana na aina mahususi.
Unaweza kuzuia hadi aina 200 za matangazo ya jumla. Ikiwa umefikia kikomo na unahitaji kuzuia aina mpya ya tangazo, utahitaji kuondoa kizuizi kwenye aina uliyozuia kwanza.
Aina nyeti
Unaweza kuzuia matangazo kutoka kwenye aina zinazohusiana na mada nyeti, kama vile Kuchumbiana, Dini au Siasa. Hii inaweza kukufaa ikiwa hungependa kuona matangazo yanayohusiana na mada nyeti.
Kumbuka kuwa aina za matangazo kuhusu Pombe na Kamari huzuiwa kwa chaguomsingi. Ukipenda, unaweza pia kuruhusu aina nyeti za matangazo kwenye chaneli yako.
Kuzuia matangazo
Kupitia Kichupo cha Matangazo kwenye Ukurasa wa Kutazama
- Kwenye kompyuta yako, ingia katika Studio ya YouTube.
- Kwenye menyu ya kushoto, bofya Chuma mapato
.
- Bofya Matangazo kwenye Ukurasa wa Kutazama.
- Bofya Aina za matangazo.
- Ili uzuie URL za watangazaji mahususi: Bofya kichupo cha URL kwenye upau mlalo katika sehemu ya juu ya ukurasa. Weka URL 1 au nyingi, ukizitenganisha kwa koma, kwenye kisanduku. Kisha ubofye ZUIA.
- Ili uzuie matangazo kulingana na aina nyeti au za jumla: Bofya kichupo husika kwenye upau mlalo katika sehemu ya juu ya ukurasa. Tafuta aina ambayo ungependa kuzuia kwenye kisanduku. Kisha ubofye ZUIA.
- Bofya HIFADHI. Mabadiliko yanapaswa kuonekana kwenye chaneli yako ndani ya saa 24.
Kupitia Kichupo cha Mipangilio
- Kwenye kompyuta yako, ingia katika Studio ya YouTube.
- Kwenye menyu ya kushoto, bofya Mipangilio
.
- Bofya Aina za matangazo.
- Ili uzuie URL za watangazaji mahususi: Bofya kichupo cha URL kwenye upau mlalo katika sehemu ya juu ya ukurasa. Weka URL 1 au nyingi, ukizitenganisha kwa koma, kwenye kisanduku. Kisha ubofye ZUIA.
- Ili uzuie matangazo kulingana na aina nyeti au za jumla: Bofya kichupo husika kwenye upau mlalo katika sehemu ya juu ya ukurasa. Tafuta aina ambayo ungependa kuzuia kwenye kisanduku. Kisha ubofye ZUIA.
- Bofya HIFADHI. Mabadiliko yanapaswa kuonekana kwenye chaneli yako ndani ya saa 24.
Kumbuka kuwa vidhibiti vya kuzuia matangazo vinatumika tu kwa matangazo yanayoonyeshwa kwenye Ukurasa wa Kutazama. Haviathiri matangazo yanayoonyeshwa kwenye Mipasho au Video Fupi. Kutokana na hali ya matangazo katika mipasho ya Video Fupi, hatuwezi kukuhakikishia kuwa aina mahususi za tangazo hazitaonekana kwenye au karibu na maudhui yako. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi matangazo yanavyoonyeshwa katika Mipasho ya Video Fupi.