Hapa chini kuna mipangilio inayopendekezwa ya kusimba upakiaji wa video zako kwenye YouTube.
Metadata: MP4- Hamna Orodha za Kubadilisha (au huenda video isichakatwe kwa usahihi)
- moov atom katika sehemu ya mbele ya faili (Kuanza kwa Haraka)
- Vituo: Stereo au Stereo + 5.1
- Kiasi cha sampuli khz96 au khz48
- Uchanganuzi endelevu (hamna kuunganisha)
- Wasifu Mkuu
- Fremu 2 za B zinazofuatana
- GOP iliyofungwa. GOP ya nusu ya kasi ya picha.
- CABAC
- Kasi ya biti yenye viwango mbalimbali. Hamna kikomo cha kasi ya biti kinachohitajika, ingawa tunatoa kasi za biti hapa chini kwa marejeleo
- Sampuli ndogo ya Chroma: 4:2:0
Maudhui yanapaswa kusimbwa na kupakiwa kwa kutumia kasi ile ile ya picha iliyotumiwa kuyarekodi.
Kasi za kawaida za picha ni pamoja na: Fremu 24, 25, 30, 48, 50, 60 kwa sekunde (kasi zingine za picha pia zinakubalika).
Maudhui yaliyounganishwa yanapaswa kutenganishwa kabla ya kupakiwa. Kwa mfano, maudhui ya 1080i60 yanapaswa kutenganishwa na kuwa 1080p30. Sehemu 60 zilizounganishwa kwa sekunde zinaweza kutenganishwa ziwe fremu 30 endelevu kwa sekunde.
Kasi za biti hapa chini zinapendekezwa kwa ajili ya vipakiwa. Kasi ya biti ya kucheza sauti hauhusiani na ubora wa video.
Kasi za picha za video zinazopendekezwa kwa vipakiwa vya SDR
Ili utazame vipakiwa vipya vya 4K kwenye 4K, tumia kivinjari au kifaa kinachotumia VP9.
Aina | Kasi ya Biti ya Video, Kasi ya Picha ya Kawaida (24, 25, 30) |
Kasi ya Biti ya Video, Kasi ya Picha ya Juu (48, 50, 60) |
---|---|---|
8K | Mbps 80 - 160 | Mbps 120 hadi 240 |
2160p (4K) | Mbps 35–45 | Mbps 53–68 |
1440p (2K) | Mbps 16 | Mbps 24 |
1080p | Mbps 8 | Mbps 12 |
720p | Mbps 5 | Mbps 7.5 |
480p | Mbps 2.5 | Mbps 4 |
360p | Mbps 1 | Mbps 1.5 |
Kasi ya biti ya video zinazopendekezwa kwa ajili ya vipakiwa vya HDR
Aina | Kasi ya Biti ya Video, Kasi ya Picha ya Kawaida (24, 25, 30) |
Kasi ya Biti ya Video, Kasi ya Picha ya Juu (48, 50, 60) |
---|---|---|
8K | Mbps 100 - 200 | Mbps 150 hadi 300 |
2160p (4K) | Mbps 44–56 | Mbps 66–85 |
1440p (2K) | Mbps 20 | Mbps 30 |
1080p | Mbps 10 | Mbps 15 |
720p | Mbps 6.5 | Mbps 9.5 |
480p |
Haitumiki |
Haitumiki |
360p | Haitumiki | Haitumiki |
Kasi ya biti ya sauti inayopendekezwa kwa vipakiwa
Aina | Kasi ya Biti ya Sauti |
---|---|
Mono | kbps 128 |
Stereo | kbps 384 |
5.1 | kbps 512 |
Uwiano wa kawaida wa YouTube kwenye kompyuta ni 16:9. Unapopakia uwiano mwingine kama vile wima au mraba, kichezaji hujirekebisha kiotomatiki ili kifae ukubwa wa video. Mipangilio hii hutoa hali bora kabisa ya utazamaji kulingana na uwiano na kifaa.
Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia uwiano na ubora wa video kwa usahihi.
Nafasi ya Rangi
Nafasi ya rangi inayopendekezwa kwa vipakiwa vya SDR
Nafasi ya Rangi | Sifa za Uhamishaji wa Rangi (TRC) | Msingi wa Rangi | Vizidishi vya solo ya Rangi |
---|---|---|---|
BT.709 | BT.709 (Thamani ya H.273: 1) | BT.709 (Thamani ya H.273 1) | BT.709 (Thamani ya H.273 1) |
YouTube husanifisha solo za rangi zinazofanana kiutendaji na misingi kabla ya kuchakata video. Kwa mfano, BT.601 na BT.709 TRC zinafanana, hivyo YouTube huziunganisha na kupata BT.709. Au, BT.601 NTSC na PAL zina solo za rangi zinazofanana kiutendaji na YouTube huziunganisha na kupata BT.601 NTSC. Vile vile, YouTube inaweza kuchukua hatua zifuatazo ili kufasiri thamani za nafasi ya rangi:
Lini | Kitendo cha YouTube |
---|---|
Nafasi ya rangi ya kipakiwa ina TRC isiyobainishwa. | Huchukulia BT.709 TRC. |
Nafasi ya rangi ya kupakia ina solo ya rangi isiyojulikana au isiyobainishwa na misingi. | Huchukulia solo ya rangi na misingi ya BT.709. |
Nafasi ya rangi ya kipakiwa huchanganya rangi za msingi na solo ya BT.601 na BT.709 na thamani zilizobainishwa. | Hutumia solo ya rangi kubatilisha misingi ya rangi na kuifanya iwe thabiti. |
Nafasi ya rangi ya kipakiwa huchanganya rangi za msingi na solo ya BT.601 na BT.709 na misingi au solo haijabainishwa. | Hutumia thamani iliyobainishwa ya rangi za msingi/solo ili kuweka na kubatilisha isiyobainishwa. |
Baada ya Usanifishaji wa Nafasi ya Rangi ya Kupakia, YouTube itakagua iwapo BT.709 au BT.601 zinalingana na zinapita kwenye nafasi ya rangu. Vinginevyo, YouTube hugeuza nafasi za rangi zisizotumika kuwa BT.709 kwa kuambatisha thamani za pikseli.
Nafasi ya rangi inayopendekezwa kwa vipakiwa vya HDR
Rejelea makala ya Kupakia video za HDR.