Unaweza kuweka orodha ya kucheza au video ya YouTube kwenye tovuti au blogu kwa kuipachika.
Ikiwa wewe ni mkufunzi, wasiliana na jukwaa lako la Teknolojia ya Elimu ili upate maelezo kuhusu jinsi ya kupachika maudhui ya YouTube kwa madarasa yako.
Kupachika video au orodha ya kucheza
- Kwenye kompyuta, nenda katika orodha ya kucheza au video ya YouTube unayotaka kupachika.
- Bofya SHIRIKI
.
- Kwenye orodha ya chaguo za Kushiriki, bofya Pachika.
- Kwenye kisanduku kinachoonekana, nakili msimbo wa HTML.
- Bandika msimbo katika tovuti yako ya HTML.
- Kwa wasimamizi wa mtandao: Utahitaji kuweka youtube.com kwenye orodha ya walioruhusiwa kukinga mtandao.
- Muhimu: Ikiwa tovuti au programu yako inalenga watoto na unapachika maudhui ya YouTube, ni lazima ubainishe mwenyewe tovuti au programu yako kwa kutumia zana hizi. Ubainishaji huu utahakikisha kuwa Google haionyeshi matangazo yaliyowekewa mapendeleo kwenye tovuti au programu hizi na baadhi ya vipengele vitazimwa katika kichezaji kilichopachikwa.
Kudhibiti chaguo za kupachika video
Washa hali ya faragha iliyoboreshwaHali ya Faragha Iliyoboreshwa ya kichezaji cha YouTube kilichopachikwa huzuia matumizi ya mara ambazo maudhui ya YouTube yaliyopachikwa yametazamwa katika kushawishi hali ya mtazamaji kuvinjari kwenye YouTube. Hii inamaanisha kwamba mwonekano wa video unaoonyeshwa katika Hali ya Faragha Iliyoboreshwa ya kichezaji kilichopachikwa hautatumika kuwekea mapendeleo hali ya utumiaji wa kuvinjari kwenye YouTube, iwe ndani ya kichezaji chako kilichopachikwa cha Hali ya Faragha Iliyoboreshwa au katika hali ya utazamaji wa mtazamaji wa YouTube.
Ikiwa matangazo yataonyeshwa kwenye video iliyoonyeshwa katika Hali ya Faragha Iliyoboreshwa ya kichezaji kilichopachikwa, matangazo hayo pia hayatawekewa mapendeleo. Pia, mwonekano wa video unaoonyeshwa katika Hali ya Faragha Iliyoboreshwa ya kichezaji kilichopachikwa hautatumika kuwekea mapendeleo utangazaji unaoonyeshwa kwa mtazamaji aliye nje ya tovuti au programu yako.
Kumbuka Sheria na Masharti ya API za YouTube na Sera za Wasanidi Programu hutumika katika ufikiaji na matumizi ya kichezaji kilichopachikwa kwenye YouTube.
Ili utumie Hali ya Faragha Iliyoboreshwa:
- Badilisha kikoa ili upachike URL kwenye HTML yako kutoka https://www.youtube.com kuwa https://www.youtube-nocookie.com.
- Kwa wasimamizi wa mtandao: Utahitaji kuweka youtube-nocookie.com kwenye orodha ya walioruhusiwa kukinga mtandao.
- Kwa utumiaji kwenye programu, tumia mfano wa Mwonekano wa Wavuti wa kichezaji kilichopachikwa. Hali ya Faragha Iliyoboreshwa inapatikana tu kwa vichezaji vilivyopachikwa kwenye tovuti.
- Muhimu: Ikiwa tovuti au programu yako inalenga watoto, ni lazima ubainishe mwenyewe tovuti au programu yako kwa kutumia zana hizi, kama inavyotakiwa na Sheria na Masharti ya API ya YouTube na Sera za Wasanidi Programu, hata ukipachika Video za YouTube kwa kutumia kichezaji cha Hali ya Faragha Iliyoboreshwa.
Mfano:
Kabla
<iframe width="1440" height="762"
src="https://www.youtube.com/embed/7cjVj1ZyzyE"
frameborder="0" allow="autoplay; encrypted-media" allowfullscreen></iframe>
Baada
<iframe width="1440" height="762" src="https://www.youtube-nocookie.com/embed/7cjVj1ZyzyE"
frameborder="0" allow="autoplay; encrypted-media" allowfullscreen></iframe>
Kumbuka: Mtazamaji akibofya au kugusa upachikaji na kuelekezwa kwenye tovuti au programu nyingine, tovuti au programu hiyo inaweza kufuatilia mwenendo wa mtazamaji kulingana na sera na masharti ya tovuti au programu hiyo.
Ili kufanya video iliyopachikwa icheze kiotomatiki, weka "&autoplay=1" kwenye msimbo wa kupachika wa video mara baada ya kitambulisho cha video (mfululizo wa herufi zinazofuata "pachika/").
Video zilizopachikwa ambazo huchezwa kiotomatiki haziongezi idadi ya utazamaji wa video.
Mfano:
<iframe width="560" height="315" src="https://www.youtube.com/embed/D6Ac5JpCHmI?&autoplay=1"frameborder="0" allowfullscreen></iframe>
Ili video ianze kucheza kutoka katika sehemu maalum, weka “?start=” kwenye msimbo wa kupachika video, ikifuatiwa na muda katika sekunde ambapo ungependa video ianze kucheza.
Kwa mfano, ikiwa unataka video ianzie kucheza ikiwa dakika 1 na sekunde 30 kwenye video, msimbo wako wa kupachika utaonekana hivi:
<iframe allowfullscreen="" frameborder="0" height="315" src="http://www.youtube.com/embed/UkWd0azv3fQ?start=90" width="420"></iframe>
Fanya manukuu yaonekane kiotomatiki kwenye video iliyopachikwa kwa kuweka "&cc_load_policy=1" katika msimbo wa kupachika video.
Unaweza pia kuchagua lugha ya manukuu kwa ajili ya video iliyopachikwa. Ili kubainisha lugha ya manukuu ya video ambayo ungependa kupachika, weka tu "&cc_lang_pref=fr&cc_load_policy=1" katika msimbo wa kupachika video.
- "cc_lang_pref" huweka lugha ya manukuu yaliyoonyeshwa kwenye video.
- "cc_load_policy=1" huwasha manukuu kwa chaguomsingi.
- "fr" inawakilisha msimbo wa lugha ya Kifaransa. Unaweza kutafuta misimbo ya lugha yenye herufi 2 katika kiwango cha ISO 639-1.
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
- Karibu na video ambayo ungependa kudhibiti, chagua Maelezo
.
- Katika sehemu ya chini, chagua ONYESHA ZAIDI.
- Batilisha uteuzi wa kisanduku cha “Ruhusu kupachika” na HIFADHI.