Kutayarisha na kudhibiti matangazo kwenye YouTube

Unaweza kuanzisha kampeni za utangazaji ukitumia kipengele cha Tangaza kwenye YouTube katika kompyuta au kifaa chako cha Android. Kutangaza husaidia kupata wafuatiliaji wapya kwenye chaneli yako, kuongeza mara za kutazamwa na ushirikishaji pamoja na kupata mibofyo zaidi katika tovuti yako.

Pata maelezo zaidi kuhusu Kutangaza kwenye YouTube au soma mwongozo wetu wa utatuzi.

Masharti ya video

Ili kutimiza masharti ya tangazo jipya, ni lazima video zikidhi vigezo vifuatavyo:

Tangazo jipya

  1. Ingia katika Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Katika menyu ya juu, chagua kichupo cha Matangazo.
  4. Bofya Tangazo Jipya katika upande wa kulia.
    • Mara ya kwanza Kutangaza: Bofya Anza kutumia.
  5. Akaunti: Chagua akaunti yako ya Google Ads kwenye menyu kunjuzi.
    • Mara ya kwanza Kutangaza: Unganisha akaunti iliyopo ya Google Ads au ubofye “Fungua akaunti mpya” ili ufungue akaunti mpya kiotomatiki.
    • Kumbuka: Akaunti zote za Google Ads zinazotumika zilizo na mipangilio kamili ya bili zitaonyeshwa hapa. Unahitaji kuchagua akaunti ya Google Ads ukitayarisha tangazo kwa mara ya kwanza tu na ni akaunti moja pekee ya Google Ads inayoweza kuunganishwa na kichupo cha "Matangazo" kwa wakati mmoja. Unaweza kutenganisha na kubadilisha akaunti za Google Ads baada ya matangazo yote kusimamishwa au kusitishwa.
  6. Lengo: Chagua lengo la tangazo lako kwenye kidokezo.
  7. Video: Video yako ya hivi majuzi huchaguliwa kwa chaguomsingi. Ili uchague video tofauti, bofya Badilisha video kisha uchague nyingine. Maelezo hutumia kiotomatiki maandishi ya sasa ya video, ambayo unaweza kuhariri pamoja na kichwa cha tangazo.
  8. Ulengaji: Bainisha lugha, nchi, umri, jinsia au mambo mahususi yanayowavutia watazamaji ambao ungependa kuwaonyesha tangazo lako.
    • Kumbuka: Video unayotangaza itaonyeshwa kwa watu ambao wana uwezekano mkubwa wa kutembelea chaneli yako). Pata maelezo zaidi kuhusu ulengaji wa kampeni za video za TrueView.
    • Kumbuka: Kwa sasa, ulengaji wa kundi lenye upendeleo maalum unapatikana tu kwenye kompyuta ya mezani.
  9. Bajeti: Bainisha bajeti na tarehe ya kuisha kwa tangazo lako. Tunapendekeza kipindi cha tangazo cha siku 10.
  10. Chagua Tangaza.

Kubadilisha tangazo

  1. Ingia katika Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Chagua Maelezo kwenye kampeni inayoendelea.
  4. Badilisha mipangilio yako kisha chagua Hifadhi.

Kusimamisha tangazo

  1. Ingia katika Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Chagua Maelezo kwenye kampeni inayoendelea.
  4. Bofya menyu kunjuzi ya “Hali” kisha chagua Sitisha tangazo.
    • Ili uendelee na tangazo bofya tena menyu kunjuzi ya “Hali” kisha chagua Linaonyeshwa.
Kumbuka: Unaweza pia kusogeza chini ili uweke “Tarehe ya mwisho” iwe leo ili usimamishe kampeni.

Kurudia tangazo

Chagua tangazo ambalo ungependa kurudia. Kisha ubofye Tangaza tena kwenye tangazo lolote la awali ili uanzishe kampeni mpya ukitumia mipangilio ile ile.

Kuelewa utendaji wa tangazo lako

Wakati unaangalia kampeni zako za Kutangaza katika Studio ya YouTube, tumia vipimo vifuatavyo ili uelewe utendaji wa kampeni mahususi:

  • Gharama: Kiasi cha pesa ambacho umetumia kwenye tangazo kufikia sasa, ambacho hakitazidi bajeti uliyoweka.
  • Maonyesho: Mara ambazo kijipicha cha kampeni yako kimeonyeshwa.
  • Mara za kutazamwa: Mara ya kutazamwa huhesabiwa mtu anapotazama maudhui yako kwa muda fulani. Soma maelezo zaidi kuhusu matangazo ya YouTube na vipimo vya mara za kutazamwa.
  • Wafuatiliaji: Idadi ya wanaofuatilia chaneli yako baada ya kutazama angalau sekunde 10 za video yako au kubofya tangazo lako ndani ya siku 3 zilizopita.
  • Mara za kutembelea tovuti: Idadi ya mibofyo kwenye kiungo cha tovuti kilichojumuishwa kwenye tangazo lako.

Wafuatiliaji na muda wa kutazama uliotokana na Kutangaza hauchangii kutimiza masharti ya Mpango wa Washirika wa YouTube.

Kumbuka: Utendaji wa matangazo yako hauathiri mapendekezo kwa njia ya halisi. Huenda ukaona vipimo tofauti vya kudumisha hadhira na asilimia ya mibofyo (CTR) katika utazamaji unaolipiwa ikilinganishwa na utazamaji usiolipiwa katika Takwimu za YouTube. Hali hii hutokea kwa sababu matangazo yanalenga kuonyesha maudhui yako kwa hadhira mpya, zinazojishirikisha kwa viwango tofauti ikilinganishwa na hadhira yako iliyopo.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Kompyuta Android

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
6129969646961793066
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
false
true
true
true
true
true
59
false
false
false
false
false