Mara nyingi TV hutumiwa kwa pamoja nyumbani. Ili kukusaidia kudhibiti faragha yako, tunakupatia vipengele vinavyokupa udhibiti zaidi wa akaunti yako na historia ya utazamaji kwenye vifaa vya pamoja.
Kulinda akaunti yako ukitumia kipengele cha kufunga akaunti
Kipengele cha kufunga akaunti hufanya akaunti yako ya YouTube kuwa ya faragha kwenye TV inayotumiwa na wengine kwa kuhitaji msimbo wa tarakimu 4 unaoweka kwenye kifaa hicho mahususi.
Kuwasha kipengele cha kufunga akaunti
Fuata hatua hizi ili uwashe kipengele cha kufunga akaunti:
1. Fikia akaunti yako kwenye menyu ya kushoto.
2. Chagua kitufe cha Mipangilio moja kwa moja kwenye akaunti yako.
3. Fuata vidokezo ili uwashe kipengele cha kufunga akaunti.
Kubadilisha msimbo wako wenye tarakimu 4
Ikiwa umesahau msimbo ulioweka wa kufunga akaunti yako, unaweza kuzima kipengele hicho kwa kuingia katika akaunti ukitumia vitambulisho vya akaunti yako ya Google.
Ili uzime kipengele cha kufunga akaunti ukitumia akaunti yako ya Google:
1. Bofya Umesahau msimbo? kwenye skrini iliyofungwa.
2. Fuata hatua ili uingie katika akaunti.
3. Baada ya kuingia katika akaunti, umezima kipengele cha kufunga akaunti kwenye kifaa hiki mahususi
Wasifu wa wanafamilia
Unapotumia programu ya YouTube kwenye TV yako, skrini ya 'Nani Anatazama' itaonyesha kiotomatiki wasifu wa Wanakikundi wote wa Familia yako kwenye Google. Ili kulinda faragha ya akaunti yako, wanafamilia huonyeshwa kama wasifu ulioondolewa kwenye akaunti. Ili mwanafamilia huyo atumie wasifu, atahitaji kuuchagua na kuingia katika akaunti akitumia vitambulisho vyake vya Akaunti ya Google. Hii inatumika tu kwa akaunti zilizo na nenosiri. Ikiwa akaunti haina nenosiri, utaingia kiotomatiki.
Kutazama kama mgeni
Iwapo ungependa kutazama YouTube bila akaunti, chagua Tazama kama mgeni. Video hupendekezwa kulingana na video ulizotazama baada ya kuondoka katika akaunti kwenye kifaa.
Kupata maelezo zaidi kuhusu chaguo za faragha na akaunti
Je, vipengele hivi vitapatikana kwenye vifaa vyote?
Je, ninawezaje kujiondoa kwenye TV, kifaa cha kutiririsha maudhui au kifaa cha michezo ya video ambacho siwezi tena kutumia?
Ninaweza kusitisha au kufuta vipi historia ya video nilizotazama?
Ninaweza kuzima vipi kipengele ambacho wasifu wa wanafamilia wangu huonekana?