Kudhibiti hali yako ya utumiaji wa kivinjari cha ndani ya programu katika YouTube kwenye iOS

Kivinjari cha ndani ya programu katika YouTube kwenye iOS kinakuwezesha kutembelea tovuti kwa urahisi bila kuondoka katika programu ya YouTube. Unaweza pia kufikia historia yako ya kuvinjari na kudhibiti mipangilio ya kivinjari chako moja kwa moja katika programu.

Kudhibiti hali ya utumiaji wa kivinjari cha ndani ya programu katika YouTube

Kufungua katika kivinjari cha nje

Ili uangalie ukurasa wowote wa wavuti kwenye kivinjari chaguomsingi cha kifaa chako:

  1. Gusa Menyu katika kona ya juu kulia.
  2. Chagua Fungua katika kivinjari cha nje.

Kuangalia historia yako ya kiungo

Unapovinjari tovuti kwenye YouTube, shughuli zako zinaweza kuhifadhiwa katika akaunti yako (kulingana na mipangilio yako ya Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu). Shughuli hii inaweza kutumiwa kukupa hali za utumiaji zilizowekewa mapendeleo pamoja na matangazo yanayokufaa zaidi.

Kwa watumiaji walioingia katika akaunti:

  • Fungua kiungo katika programu ya YouTube ili ufungue kivinjari cha ndani ya programu.
  • Katika sehemu ya juu kulia, gusa Menyu, kisha Angalia Historia ya Kiungo .
  • Hapa unaweza kuangalia historia yako ya kivinjari cha ndani ya programu, pamoja na historia ya mambo uliyotafuta na kutazama kwenye YouTube. Ili ufikie shughuli zako:
    • Vinjari shughuli zako, zikiwa zimepangwa kulingana na tarehe na wakati.
    • Ili upate shughuli mahususi, katika sehemu ya juu, tumia upau wa kutafutia na vichujio.

Kufuta shughuli zako

Unapoangalia historia yako ya kiungo, unaweza kuchagua kufuta shughuli zote au vipengee mahususi vya shughuli.

Ili ufute shughuli zote:

  • Katika sehemu ya juu ya skrini inayoonyesha shughuli zako, gusa Futa.
  • Gusa Kila wakati.
  • Gusa Endelea kisha Futa.

Ili ufute vipengee mahususi vya shughuli:

  • Sogeza chini kwenye shughuli zako.
  • Tafuta kipengee ambacho ungependa kufuta. Unaweza kupata kipengee kwa njia kadhaa tofauti, ikiwa ni pamoja na:
    • Kuvinjari kulingana na tarehe.
    • Kutafuta au kutumia vichujio.
  • Kwenye kipengee ambacho ungependa kufuta, gusa Futa.

Kudhibiti data yako

Unaweza kubadilisha shughuli zinazohifadhiwa.

Kwa watumiaji walioingia katika akaunti:

  • Fungua kiungo katika programu ya YouTube ili ufungue kivinjari cha ndani ya programu.
  • Katika sehemu ya juu kulia, gusa Menyu kisha Dhibiti shughuli zangu .
  • Wakati umewasha Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu, unaweza kupata hali zilizowekewa mapendeleo na matangazo yanayokufaa.
  • Ili uzime Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu
    • Gusa Zima kisha chagua Kuzima au Kuzima na kufuta shughuli.
    • Ukichagua Kuzima na kufuta shughuli, fuata hatua ili uchague na uthibitishe shughuli ambazo ungependa kufuta.

Kuvinjari faraghani

Wakati unavinjari faraghani kwenye YouTube katika kifaa chako cha mkononi, programu ya YouTube hufanya kazi kana kwamba hujaingia katika akaunti. Shughuli zako za kivinjari cha ndani ya programu hazitaathiri hali yako ya utumiaji wa YouTube.

Shughuli yako katika kipindi hiki haitaunganishwa na akaunti yako. Matumizi ya data hufuata Sera ya Faragha ya Google. Ukizima hali ya faraghani, utarejea kwenye akaunti ya mwisho uliyotumia kabla ya kuwasha hali ya Faraghani. Pia, ikiwa hujatekeleza shughuli yoyote kwa zaidi ya dakika 90, Kipindi chako faraghani kitaisha. Kisha utarejeshwa kwenye akaunti ya mwisho uliyotumia. Utakapofungua YouTube tena, utapata ujumbe wa kukufahamisha kuwa hauko tena Faraghani.

Unapojaribu kufikia historia ya kiungo, utaombwa uingie katika akaunti ili ukamilishe kitendo hicho.

Tumejitolea kukupa maelezo dhahiri na udhibiti wa data yako. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi Google inavyotumia data ya shughuli uliyohifadhi na inavyoihifadhi kwa faragha.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
1826632348213527991
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
false
true
true
true
true
true
59
false
false
false
false