Tuna aina kadhaa za uanachama wa YouTube unaolipiwa ili kusaidia kuboresha hali yako ya utumiaji kwenye YouTube. Bofya viungo vilivyo hapa chini ili upate maelezo zaidi kuhusu huduma zetu za uanachama unaolipiwa.
Vifurushi
Vifurushi vya Binafsi vya Mwezi
Vifurushi vya binafsi vimepangwa ili vitumiwe na mtumiaji mmoja na haviwezi kutumiwa na watumiaji wengi katika akaunti moja. Usajili husasishwa kila mwezi.
Kujisajili kwenye uanachama wa YouTube Premium au wa YouTube Music Premium
Kupata uanachama wa Premium Lite kwenye YouTube
Vifurushi vya Kulipia Mapema
Vifurushi vya kulipia mapema hununuliwa mapema kwa kipindi mahususi na havisasishwi kiotomatiki. Vifurushi hivi vinapatikana tu kwa watumiaji binafsi. Unaweza kutumia kifurushi cha kulipia mapema kwa hadi miezi 24. Huwezi kusitisha vifurushi vya kulipia mapema.
Kujisajili kwenye kifurushi cha mwaka cha YouTube Premium au YouTube Music Premium
Vifurushi vya Watu Wengi
Vifurushi vya watu wengi vinapatikana kwenye YouTube Premium na YouTube Music Premium. Tuna vifurushi vya watu wengi ambavyo ni, Kifurushi cha familia au Kifurushi cha Watu Wawili, kwa wanafamilia wanaoishi katika nyumba moja na msimamizi wa familia. Kifurushi cha familia kina manufaa ya uanachama ya hadi watu 6 na Kifurushi cha watu wawili kina manufaa ya uanachama ya watu 2.
Kuanzisha kifurushi cha familia cha YouTube Premium au cha YouTube Music Premium
Kuanzisha Kifurushi cha watu wawili cha YouTube Premium au cha YouTube Music Premium
Kifurushi cha Wanafunzi
Uanachama wa wanafunzi unapatikana kwa wanafunzi wa muda wote kwenye taasisi za elimu ya juu zilizoidhinishwa, unatumika kwa hadi miaka 4 na unategemea kuthibitishwa kwa hali ya kuwa mwanafunzi kila mwaka na mtoa huduma mwingine wa uthibitishaji.
Kupata uanachama wa wanafunzi wa YouTube Premium
Maelezo ya Ziada
Maeneo ambako uanachama wa Premium unapatikana
Pata maelezo kuhusu majaribio na ofa za YouTube Premium
Njia za kulipa zinazokubaliwa kwenye YouTube Premium
Kurekebisha hitilafu za kujisajili kwenye YouTube Premium na YouTube Music Premium