Kufungua chaneli ya YouTube

Unaweza kutazama, kupenda video na kufuatilia chaneli ukitumia Akaunti ya Google. Unahitaji chaneli ya YouTube ili upakie video, utoe maoni au utayarishe orodha. Isipokuwa ufungue chaneli, hutaonekana kwa umma kwenye YouTube.

Jinsi ya Kufungua Chaneli ya YouTube na Kuiwekea Mapendeleo (Mambo ya Msingi kwa Watayarishi)

Kufungua chaneli binafsi

Fuata maagizo haya ili ufungue chaneli ambayo ni wewe tu unaweza kuidhibiti.

  1. Ingia katika YouTube ukitumia kompyuta au tovuti ya kifaa cha mkononi.
  2. Bofya picha yako ya wasifu kisha Mipangilio .
  3. Nenda katika sehemu ya Akaunti kisha uchague Weka au udhibiti chaneli.
  4. Bofya Fungua chaneli .
  5. Chagua picha ya wasifu, andika jina na Utambulisho wako.
  6. Bofya Fungua chaneli.

Kufungua chaneli ukitumia jina la biashara au jina lingine

Fuata maagizo haya ili ufungue kituo ambacho kinaweza kuwa na zaidi ya msimamizi au mmiliki mmoja.

Unaweza kuunganisha kituo chako na Akaunti ya Biashara iwapo ungependa kutumia jina tofauti kwenye YouTube badala ya jina unalotumia kwenye Akaunti yako ya Google. Pata maelezo zaidi kuhusu Akaunti za Biashara.

  1. Ingia katika YouTube ukitumia kompyuta au tovuti ya kifaa cha mkononi.
  2. Nenda kwenye orodha ya kituo chako.
  3. Chagua kufungua chaneli mpya au kutumia Akaunti iliyopo ya Biashara:
    • Ili ufungue chaneli, bofya Fungua chaneli mpya.
    • Ili ufungue chaneli ya YouTube ya Akaunti ya Biashara ambayo tayari unasimamia, chagua Akaunti ya Biashara kwenye orodha. Iwapo tayari Akaunti ya Biashara ina chaneli, huwezi kufungua mpya. Unapochagua Akaunti ya Biashara kwenye orodha, utaelekezwa kwenye chaneli hiyo.
  4. Chagua picha ya wasifu, jina na Utambulisho.
  5. Bofya Fungua chaneli. Hatua hii itafungua Akaunti mpya ya Biashara.
  6. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuweka wadhibiti na wamiliki wa chaneli.
Kumbuka: Huenda hutaweza kufungua chaneli iwapo unatumia YouTube katika hali ya matumizi yanayosimamiwa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
13673459536060416168
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
false
true
true
true
true
true
59
false
false
false
false