Fungua Kituo cha YouTube

Unaweza kutazama na kupenda video pamoja na kufuatilia vituo ukitumia Akaunti ya Google. Lakini bila kuwa na kituo cha YouTube, hutaonekana hadharani kwenye YouTube. Hata ukiwa na Akaunti ya Google, unahitaji kufungua kituo cha YouTube ili upakie video, utoe maoni au uunde orodha za kucheza.

Unaweza kufungua kituo chako kwenye tovuti ya YouTube au tovuti ya YouTube ya kifaa cha mkononi.

Kumbuka: Huenda kipengele hiki kisipatikane kwa matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube. Pata maelezo zaidi.

Kuanza | Jinsi na sababu ya kuingia katika akaunti kwenye YouTube na kufungua chaneli ya YouTube

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Kufungua kituo binafsi

Fuata maagizo haya ili ufungue kituo ambacho ni wewe tu unayeweza kudhibiti kwa kutumia Akaunti yako ya Google.

  1. Ingia katika akaunti kwenye YouTube ukitumia kompyuta au tovuti ya kifaa cha mkononi.
  2. Bofya picha yako ya wasifu kishaFungua kituo.
  3. Utaombwa ufungue kituo.
  4. Kagua maelezo (yaliyo na jina na picha ya Akaunti yako ya Google) kisha uthibitishe ili ufungue kituo chako.
Kumbuka: Katika hali fulani, kama vile unapounda kituo kupitia mbinu kama vile kuchapisha maoni kwenye kifaa cha mkononi, YouTube inaweza kukupatia kiotomatiki kitambulishi kulingana na jina la kituo chako ulilochagua. Huenda kukawa na matukio ambapo utapewa kinasibu kitambulishi chako iwapo jina la kituo ulilochagua halitaweza kubadilishwa kuwa kitambulishi. Mara zote unaweza kuangalia na kuhariri kitambulishi kwenye Studio au kwa kwenda kwenye youtube.com/handle.

Kufungua kituo kwa kutumia jina la biashara au jina lingine

Fuata maagizo haya ili ufungue kituo ambacho kinaweza kuwa na zaidi ya msimamizi au mmiliki mmoja.

Unaweza kuunganisha kituo chako na Akaunti ya Biashara iwapo ungependa kutumia jina tofauti kwenye YouTube badala ya jina unalotumia kwenye Akaunti yako ya Google. Pata maelezo zaidi kuhusu Akaunti za Biashara.

  1. Ingia katika akaunti kwenye YouTube ukitumia kompyuta au tovuti ya kifaa cha mkononi.
  2. Nenda kwenye orodha ya kituo chako.
  3. Chagua kufungua kituo kipya au kutumia Akaunti iliyopo ya Biashara:
    • Fungua kituo kwa kubofya Fungua kituo kipya.
    • Fungua kituo cha YouTube cha Akaunti ya Biashara ambayo tayari unasimamia kwa kuchagua Akaunti ya Biashara kwenye orodha. Iwapo tayari Akaunti hii ya Biashara ina kituo, huwezi kufungua kipya. Unapochagua Akaunti ya Biashara kwenye orodha, utaelekezwa kwenye kituo hicho.
  4. Jaza maelezo ili ukipe jina kituo chako kipya. Kisha, bofya Fungua. Hatua hii itafungua Akaunti mpya ya Biashara.
  5. Ili umwongeze msimamizi wa kituo, fuata maagizo ya kubadilisha wasimamizi na wamiliki wa kituo.

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia kituo kupitia jina la biashara au jina lingine kwenye YouTube.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8513463611924919701
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false