Kutayarisha video ukitumia violezo kwenye YouTube Create

Tayarisha video ukitumia kipengele cha violezo cha YouTube Create. Violezo vya YouTube Create ni miundo ya video iliyobuniwa na kuwekwa mapema inayokusaidia kutayarisha video za aina kama vile mapishi, safari na mitindo kwa haraka na kwa urahisi. Kipengele cha violezo kinakupa urahisi na uwekaji kamili wa mapendeleo kwenye programu ya YouTube Create ili utayarishe video zako katika mtindo unaopendelea bila vikomo vya zana za violezo za zamani.

✨NEW✨ Templates in YouTube Create

YouTube Create inapatikana kwenye simu za Android ambazo zina angalau RAM ya 4G. Huenda programu hii ikapatikana kwenye vifaa vingine katika siku zijazo.

Kutayarisha video ukitumia kipengele cha violezo

  1. Katika programu ya YouTube Create, sogeza kwenye ukurasa wa kwanza ili uvinjari violezo vyote tofauti.
  2. Gusa Angalia vyote ili uone violezo vyote kwenye aina.
  3. Ukishapata kiolezo anachopenda, gusa Tumia Kiolezo.
  4. Kisha, kwenye matunzio yako, chagua picha, video au maudhui uliyopakia hapo awali ili uweke kwenye mradi wako.
    • Kumbuka: Gusa Kishale kilicho karibu na Matunzio katika sehemu ya juu ya skrini ili upakie maudhui kutoka kwenye programu nyingine katika kifaa chako.
  5. Gusa Pakia ili uweke picha na video kwenye mradi wako.
  6. Angalia toleo la kukagua kiolezo chenye maudhui uliyopakia.
  7. Gusa Zana ya kuhariri klipu ili uchague sehemu sahihi ya klipu za kuweka kwenye kiolezo.
  8. Gusa Hamisha au uende kwenye Kihariri cha YouTube Create ili utumie kifurushi kamili cha zana za kuhariri.
  9. Gusa Pakia baada ya kuhamisha ili upakie video uliyomaliza kuhariri kwenye YouTube.
Kumbuka: Mradi huanzishwa na kuhifadhiwa kiotomatiki katika Kihariri cha YouTube Create au baada ya kuhamisha.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
7657139626823796545
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
false
true
true
true
true
true
59
false
false
false
false