Kuelewa ukaguzi wa ziada wa uchumaji wa mapato

Advertiser-friendly Content Guidelines & Yellow Monetization Icons

Ili kuboresha usahihi wa maamuzi yetu kuhusu aikoni ya manjano na kufanya video zako zichume mapato kwa haraka, tunafanya majaribio kwa kutuma kiotomatiki video zinazopata ukadiriaji wa “Matangazo machache au hamna matangazo” ili zifanyiwe ukaguzi wa ziada unaoweza kukamilishwa na binadamu.

YouTube inaelewa umuhimu wa maamuzi sahihi ya uchumaji wa mapato. Ukaguzi wa ziada unalenga kuboresha uthabiti na usahihi wa tathmini za uchumaji wa mapato, kupunguza haja ya kukata rufaa na kukupa hakika zaidi katika hali ya uchumaji wa mapato kwenye video yako.

Utaratibu wa ukaguzi wa ziada ni upi?

Unapopakia video, mifumo yetu huikagua kwa kuilinganisha na mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji wakati huo unaweza kuona aikoni ya saa ya kijivu inayosema 'inakaguliwa'. Katika hali nyingi, aikoni hii itabadilika iwe ya kijani ndani ya dakika chache. Hata hivyo, ikiwa mwanzoni video imekabidhiwa hali ya uchumaji wa mapato ya 'Matangazo machache au hamna matangazo' (ambayo pia inaitwa “aikoni ya manjano”), itaelekezwa kiotomatiki kwenye ukaguzi wa ziada na aikoni ya saa ya kijivu inayosema 'inakaguliwa' itasalia hadi ukaguzi utakapomilika. Wakati huu, pia utaona ujumbe kwenye Studio ya YouTube unaosema 'Ukaguzi wa ziada.' Mchakato huu utakamilika ndani ya saa chache katika video nyingi, ingawa unaweza kuchukua hadi saa 24.

Hata baada ya ukaguzi huu wa ziada, bado una uwezo wa kukata rufaa dhidi ya uamuzi iwapo hukubali. Kupitia mchakato wetu wa ukaguzi wa ziada, tuna hakika zaidi katika usahihi wa maamuzi yetu kuhusu uchumaji wa mapato. Hata hivyo, bado tungependa kuhakikisha kuwa watayarishi wana chaguo la kukata rufaa.

Tunakuhimiza upakie maudhui yako katika hali ya “Hayajaorodheshwa” au “ya faragha” mapema iwezekanavyo na usiyafanye ya umma hadi mchakato wa ukaguzi wa ufaafu wa kuwekwa matangazo utakapokamilika.

Manufaa ya ukaguzi wa ziada ni yapi?

  • Hakika Zaidi katika Uchumaji wa Mapato: Maamuzi sahihi zaidi ya awali kuhusu uchumaji wa mapato yanayosababisha uthabiti wa hali ya juu kwenye ukadiriaji wa video.
  • Idadi ya Rufaa Iliyopungua: Kupungua kwa haja ya kutuma mwenyewe ombi la ukaguzi wa ziada, hivyo kuokoa muda na juhudi.
  • Kuongezeka kwa Fursa za Uchumaji wa Mapato: Uwezekano ulioboreshwa wa kuchuma mapato kwenye maudhui yako kikamilifu kutoka mwanzo.

Video za Faragha

Tunafahamu kuwa mara nyingi watayarishi hupakia video zikiwa “za faragha” kwanza kabla ya kuzifanya ziwe za umma. Ili kuharakisha mchakato wa uchumaji wa mapato, tutatekeleza pia ukaguzi wetu wa ziada kwenye video mpya zilizopakiwa zikiwa za faragha. Kufanya hivyo kutatoa uamuzi wa haraka na sahihi zaidi kwenye kikundi kikubwa zaidi cha watayarishi kwa kukuwezesha kukamilisha ukaguzi wowote wa ziada kabla ya kuchapisha, hivyo kuongeza kiwango cha hakika katika mipangilio yako ya uchumaji wa mapato kuanzia unapofanya video yako iwe ya umma.

YouTube imejitolea kukupa zana na usaidizi unaohitaji ili utayarishe maudhui na uchume mapato kwa ufanisi. Ukaguzi wa ziada unaonyesha wajibu wetu wa kuboresha hali ya uchumaji wa mapato kwa watayarishi. Ikiwa una maswali ya ziada, tafadhali wasiliana na majukwaa ya jumuiya au timu yetu ya usaidizi.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Swali: Kwa nini YouTube inaongeza hatua za ziada kwenye ukaguzi wa ufaafu wa kuwekwa matangazo?

Jibu: Tunafahamu jinsi ilivyo muhimu kuweza kuchuma mapato kutokana na video baada tu ya kuichapisha, wakati utazamaji unaanza kuwa juu. Ili kufanikisha hili kwa usahihi wa juu na kupunguza usumbufu wa kukata rufaa, tunaweka hatua za ziada katika ukaguzi wa ufaafu wa kuwekwa matangazo unapopakia video. Hii inamaanisha kuwa utapokea maamuzi ya kuaminika zaidi ya uchumaji wa mapato, hivyo kupunguza ucheleweshaji na juhudi zinazohusishwa na ukataji wa rufaa, kwa hivyo unaweza kuanza kuchuma mapato kwa haraka zaidi.

Swali: Je, sasa nitasubiri saa 24 ili nione aikoni ya uchumaji wa mapato? Huo ni muda mrefu!

Jibu: Hapana. Maudhui mengi tunayokagua hupokea uamuzi ndani ya dakika chache na hilo halipaswi kubadilika. Kitakachobadilika ni kuwa kwa sehemu ndogo ya video, tutaongeza ukaguzi wa ziada ili kuhakikisha usahihi. Ukaguzi huu unaweza kuchukua muda mrefu zaidi kabla ya kutoa uamuzi wa awali, lakini lengo ni kutoa uamuzi sahihi zaidi. Hali hii inaweza kusaidia kuepuka rufaa zisizohitajika na kukuwezesha kuchuma mapato kwenye maudhui yako kwa haraka zaidi. Hapo awali, video zilizopata aikoni ya manjano zilihitaji kukatiwa rufaa ili zifanyiwe ukaguzi wa ziada, hatua iliyorefusha muda ambao mtayarishi alihitaji kusubiri ili aweze kuchuma mapato kutokana na video yake. Sasisho hili linalenga kuwasaidia watayarishi kupata uamuzi sahihi kuhusu uchumaji wa mapato kwa haraka na kupunguza haja ya kukata rufaa.

Swali: Ninapaswa kufanya nini iwapo video yangu imekuwa katika hatua ya “inakaguliwa” kwa muda mrefu?

Jibu: Watayarishi hawahitaji kuchukua hatua yoyote iwapo video yao imesalia katika hatua ya “inakaguliwa” kwa hadi saa 24. Utaona kuwa hali ya uamuzi kuhusu uchumaji wako wa mapato itasalia kuwa “inakaguliwa” hadi uamuzi wa mwisho utakapopatikana. Baada ya uamuzi kufanywa, tutakufahamisha kupitia barua pepe na uamuzi kuhusu uchumaji wa mapato utaonekana kwenye kichupo cha maudhui katika Studio.

Swali: Je, nitachuma mapato kidogo iwapo video yangu itasalia katika hali ya “inakaguliwa” kwa hadi saa 24?

Jibu: Lengo la sasisho hili ni kuwasaidia watayarishi kuchuma mapato kwa haraka zaidi, kwa kuboresha usahihi wa maamuzi yetu kuhusu uchumaji wa mapato. Tunafahamu jinsi ilivyo muhimu kuweza kuchuma mapato kutokana na video baada ya kuichapisha, wakati utazamaji unaanza kuwa juu. Hapo awali, video zilizopata aikoni ya manjano zilihitaji kukatiwa rufaa ili zifanyiwe ukaguzi wa ziada, hatua iliyorefusha muda ambao mtayarishi alihitaji kusubiri ili aweze kuchuma mapato kutokana na video yake. Sasisho hili linalenga kuwasaidia watayarishi kupata uamuzi sahihi kuhusu uchumaji wa mapato kwa haraka na kupunguza haja ya kukata rufaa. Kama kawaida, tunapendekeza usubiri ukaguzi ukamilike kabla ya kufanya video yako kuwa ya umma ili uongeze uwezo wa kuchuma mapato wa video yako.

Swali: Kwa nini YouTube inakagua video ambazo mipangilio yake ya uonekanaji ni “ya faragha”? Itakuwaje iwapo sitaki video hizi zikaguliwe kama zinafaa kuwekwa matangazo?

Jibu: Video za faragha hazitaonekana kwenye kichupo cha Video katika ukurasa wa kwanza wa chaneli yako, hata hivyo mifumo ya YouTube pamoja na wahakiki wanadamu wanaweza kukagua video za faragha ili kubaini hakimiliki, ufaafu wa kuwekwa matangazo na hatua nyingine za kuzuia matumizi mabaya.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
9249152725806662164
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
false
true
true
true
true
true
59
false
false
false
false
false