Mipangilio ya kuruhusu ufikiaji wa maarifa kuhusu chaneli huwapa watayarishi wanaotimiza masharti ya Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) njia rahisi ya kuruhusu kufikiwa kwa maarifa yaliyojumlishwa kuhusu chaneli katika Studio ya YouTube ili kusaidia watangazaji, chapa na mifumo mingine kubaini iwapo chaneli ya mtayarishi inafaa kwa hadhira yao. Hii inaweza kusababisha kuongezeka kwa fursa za kuchuma mapato kutoka kwenye matangazo, ufadhili wa kibiashara na mipango ya washirika wa ununuzi.
Maarifa haya yaliyojumlishwa yatajumuisha takwimu za chaneli, uchanganuzi wa hadhira na maarifa kuhusu utendaji wa mpango wa washirika wa Ununuzi kwenye YouTube (ikiwa upo kwenye mpango wa washirika wa Ununuzi kwenye YouTube). Kwa chaguomsingi mipangilio hii imezimwa na watayarishi wana udhibiti kamili wa kuiwasha na kuizima wakati wowote. Ili kuanza, watayarishi watahitaji kuthibitisha chaguo zao za kuwasha mipangilio ya kuruhusu ufikiaji wa maarifa kuhusu chaneli katika Studio ya YouTube.
- Fursa zaidi za kuchuma mapato: Kuruhusu maarifa kuhusu chaneli yafikiwe husaidia watangazaji, chapa na mifumo mingine kugundua watayarishi, jambo linaloweza kusababisha fursa zaidi za kuchuma mapato kama vile matangazo yenye mapato ya kiwango cha juu, ufadhili wa kibiashara pamoja na ofa za ununuzi kutoka kwa washirika.
- Maarifa ya kina: Hutoa vipimo vya jumla vya chaneli kwenye mifumo mbalimbali inayotumiwa na watangazaji, chapa na mifumo mingine ili kudhibiti kampeni na kuwashirikisha watayarishi.
- Kuruhusu ufikiaji kwa urahisi: Ili uanze kuruhusu maarifa kuhusu chaneli yako yafikiwe, nenda tu kwenye “Mipangilio ya kina” ya chaneli yako katika Studio ya YouTube kisha ujijumuishe.
Kutimiza masharti
Mipangilio ya kuruhusu ufikiaji wa maarifa kuhusu chaneli inapatikana kwa watayarishi waliojiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube kote duniani katika Studio ya YouTube kwenye kompyuta ya mezani, isipokuwa katika Chaneli Rasmi za Wasanii (“OAC”).
Kuwasha mipangilio ya kuruhusu ufikiaji wa maarifa kuhusu chaneli
Unaweza kuruhusu maarifa kuhusu chaneli yako yafikiwe kwa kuwasha mipangilio katika Studio ya YouTube. Ikiwa wakati wowote ungependa kuacha kuruhusu maarifa kuhusu chaneli yako yafikiwe, unaweza kuzima mipangilio. Ukizima mipangilio hii, huenda bado ukatambulika kutokana na data yako ya umma (k.m., jina la chaneli, idadi ya wanaofuatilia, mara za kutazamwa) kuonekana kwa watangazaji, chapa na mifumo mingine.
- Ingia katika Studio ya YouTube kwenye Kompyuta ya mezani.
- Katika sehemu ya chini kushoto, bofya Mipangilio
.
- Katika sehemu ya kushoto, bofya Chaneli
Mipangilio ya kina.
- Chini ya sehemu ya “Kuruhusu ufikiaji wa maarifa kuhusu chaneli” teua kisanduku cha Ruhusu watangazaji, chapa na mifumo mingine ione maarifa kuhusu chaneli ili kupata fursa za kuchuma mapato.
- Kumbuka: Ili uzime mipangilio, acha kuteua kisanduku.
- Bofya Hifadhi.
Wanaoruhusiwa na YouTube kufikia maarifa
YouTube huruhusu watangazaji, chapa na mifumo mingine ione maarifa ya chaneli yaliyojumlishwa. Maarifa kuhusu chaneli huruhusiwa kufikiwa kwenye zana zilizoidhinishwa na Google ikiwa ni pamoja na, lakini si tu Ushirika na Watayarishi wa YouTube, Google Ads Insights Finder na Google Merchant Center.
Maarifa yanayoruhusiwa kufikiwa
Mipangilio ya kuruhusu ufikiaji wa maarifa kuhusu chaneli huruhusu watangazaji, chapa na mifumo mingine kufikia takwimu za chaneli, demografia za hadhira na utendaji wa ununuzi. Watayarishi wanaweza kuona pia maarifa haya kama ilivyobainishwa hapa chini.
Takwimu za chaneli
| Mahali | Vipimo |
| Takwimu za YouTube |
|
| Ukurasa wa kwanza wa chaneli au uliotolewa moja kwa moja na mtayarishi |
|
Uchanganuzi wa hadhira
| Mahali | Vipimo |
| Takwimu za YouTube |
|
| Muhtasari wa Takwimu |
|
Utendaji wa ununuzi
| Mahali | Vipimo |
| Takwimu za YouTube |
|
| Video mahususi zilizowekewa lebo |
|
Maswali Yanayoulizwa Sana
Kama mtayarishi, ninaweza kuona wapi data ambayo watangazaji, chapa na mifumo mingine inaruhusiwa kufikia?
Je, kuruhusu ufikiaji wa maarifa kuhusu chaneli ni tofauti na ufikiaji kwa washirika wa biashara?
Ndiyo, kuruhusu ufikiaji wa maarifa kuhusu chaneli kunalenga kusaidia watangazaji, chapa na mifumo mingine kugundua na kushirikiana na watayarishi kwa kuruhusu takwimu za chaneli, uchanganuzi wa hadhira na utendaji wa ununuzi ufikiwe (sehemu ya Mpango wa washirika wa Ununuzi kwenye YouTube).
Kwa upande mwingine, ufikiaji wa mshirika wa biashara unaoanzishwa na mtayarishi au chapa unalenga watayarishi ili waweze kuruhusu vipimo vya utendaji wa video vifikiwe na kuruhusu chapa itumie video hiyo katika tangazo la ushirika. Pata maelezo zaidi kuhusu ufikiaji kwa washirika wa biashara.Je, ninapaswa kujijumuisha katika kipengele cha kuruhusu ufikiaji wa maarifa kuhusu chaneli hata ikiwa tayari nimetoa idhini yangu kupitia Ushirika na Watayarishi wa YouTube?
Je, kuruhusu ufikiaji wa maarifa kuhusu chaneli kutachukua nafasi ya Sheria na Masharti ya Ushirika na Watayarishi wa YouTube na Ununuzi ambayo nilikubali hapo awali?