Mwongozo na sera za mashindano kwenye YouTube

Mashindano yote yanayoendeshwa kwenye YouTube au yanayotumia YouTube yanasimamiwa na kanuni zilizo hapa chini. Pia, mashindano yako hayapaswi kuendeshwa au kutekelezwa kwa njia inayokiuka Sera yetu ya Faragha. Maudhui pia hayapaswi kukiuka Sheria na Masharti ya YouTube au Mwongozo wa Jumuiya.

YouTube hairuhusu mashindano yaendeshwe kupitia makundi ya matangazo. Ikiwa mashindano yanafuata kanuni zilizo hapa chini, unaweza kutumia mashindano kupitia maudhui yako kwenye mfumo.

I. Masharti na Vizuizi vya Jumla:

  1. Unawajibikia kikamilifu mashindano yako.
  2. Mashindano yako kwenye YouTube lazima yatii sheria na kanuni zote husika za nchi, jimbo na eneo, ikiwa ni pamoja na vikwazo vya Marekani.
  3. Mashindano yako hayapaswi kukiuka au kuhimiza ukiukaji wa haki zozote za wengine au kushiriki kwenye shughuli yoyote isiyo halali.
  4. Hupaswi kumwomba mtazamaji akupe haki zote au kuhamishia umiliki wa nafasi yake kwako.
  5. Mashindano yako lazima yawe ya kujiunga bila malipo (usisahau kufuata sheria za michezo ya bahati nasibu za mahali uliko!).
  6. Wewe na mtu mwingine yeyote hampaswi kubadilisha vipimo kwenye huduma ya YouTube ili kuwakilisha kwa uongo takwimu halisi za watazamaji kwenye huduma ya YouTube. Vipimo hivi vinajumuisha idadi ya mara za kutazamwa, kupendwa, kutopendwa au wafuatiliaji.
  7. Hupaswi kushirikisha au kuhusisha YouTube na mashindano yako bila kupata idhini ya mapema ya YouTube kupitia maandishi. Kanuni hii hairuhusu, miongoni mwa mifano mingine, kueleza kwa uwazi au kufanya kitu chochote kinachoashiria kuwa YouTube inahusika au imeidhinisha mashindano yako kwa njia yoyote.

II. Kanuni Zako Rasmi za Mashindano:

  1. Lazima ubainishe kikundi cha "Kanuni Rasmi" ambazo:
    a. zinajumuisha viungo vya kuunganisha kwenye Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube na ubainishe kuwa washiriki ambao hawatii kanuni wataondolewa.
    b. zinaeleza ufumbuzi wote unaohitajika na sheria na kanuni zote husika za nchi, jimbo na eneo, ikiwa ni pamoja na vikwazo vya Marekani.
    c. zinatii kikamilifu na zinalingana na Sheria na Masharti ya YouTube.
  2. Mashindano yako lazima yafanyike, na zawadi zote kutolewa kama inavyoelezwa kwenye Kanuni zako Rasmi.
  3. Unawajibika kwa kanuni zako na vipengele vyote vya utekelezaji wa mashindano yako.
  4. Kanuni zako lazima zieleze kwa uwazi kuwa YouTube si mfadhili wa mashindano yako na kueleza watazamaji kuwa wanapaswa kuondolewa YouTube dhima yoyote inayohusiana na mashindano yako.
  5. Lazima ujumuishe ilani ya faragha inayotii sheria kwenye Kanuni zako Rasmi. Ilani hii inaeleza jinsi utakavyotumia data yoyote binafsi utakayokusanya kwa ajili ya mashindano na kutii matumizi hayo.

Kanusho: Sisi si mawakili wako na maelezo yaliyotolewa hapa si ushauri wa kisheria. Tunayatoa kwa madhumuni ya maelezo na tunapendekeza utafute ushauri katika eneo la mamlaka uliko kuhusu kuendesha mashindano kwa njia halali.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
16590543912449807448
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false