Ili uingie katika akaunti ya YouTube, utahitaji kufungua Akaunti ya Google. Akaunti ya Google inakuruhusu utumie vipengele vingi vya YouTube ikiwa ni pamoja na Kupenda, Kufuatilia, Tazama Baadaye na Historia ya Video Ulizotazama.
Ukishaingia katika YouTube kupitia Akaunti yako ya Google, unaweza kufungua chaneli ya YouTube kwenye akaunti yako. Chaneli za YouTube zinakuruhusu upakie video, utoe maoni na kutunga orodha za kucheza.