Maelezo ya sauti ni masimulizi ambayo huwezesha hadhira yako ifikie maudhui ya video. Maelezo ya sauti huelezea kinachoendelea kwenye skrini wakati wa mapumziko ya kawaida katika sauti, ili hadhira yako ielewe vyema na iweze kufuatilia.
Kumbuka: Huenda usiweze kufikia maelezo ya sauti. Hata hivyo, watayarishi walio na idhini ya kufikia kipengele cha sauti ya lugha nyingi wanaweza kuweka maelezo ya sauti. Pata maelezo kuhusu kipengele cha sauti ya lugha nyingi.
Kupakia maelezo mapya ya sauti
- Ingia katika Studio ya YouTube kwenye kompyuta yako.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Lugha
.
- Bofya video ambayo ungependa kuhariri.
- Chagua lugha yako.
- Kumbuka: Ili uweke sauti ya ufafanuzi, unahitaji kuwa tayari umepakia sauti halisi au iliyotafsiriwa katika lugha ya sauti ya ufafanuzi.
- Karibu na ‘Sauti ya ufafanuzi,’ bofya Weka.
- Bofya Chagua faili.
- Chagua faili ya kupakia. Ni lazima faili iwe katika aina ya faili inayotumiwa ya sauti pekee na iwe na takribani urefu sawa na video yako.
- Bofya Chapisha ukiwa tayari kupakia sauti yako.
Kubadilisha faili za sauti ulizopakia awali
Ikiwa ulipakia maelezo ya sauti na ungependa kuyabadilisha uweke maelezo mapya ya sauti:
- Ingia katika Studio ya YouTube kwenye kompyuta yako.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Lugha
.
- Bofya video ambayo ungependa kuhariri.
- Chagua lugha ambayo ungependa kufuta.
- Baada ya kufungua lugha, nenda kwenye ‘Sauti ya Ufafanuzi.’
- Bofya
Futa kwenye lugha ambayo ungependa kubadilisha.
- Rudia hatua za kupakia maelezo mapya ya sauti.
lli kuhakikisha kuwa video zako zinafikiwa na watazamaji wengi, pata maelezo zaidi kuhusu kuongeza manukuu na kutafsiri majina na maelezo ya video.