Kuanzisha Kifurushi cha watu wawili cha YouTube Premium au cha YouTube Music Premium

Pata Kifurushi cha YouTube cha watu wawili ili utumie YouTube Premium au YouTube Music Premium pamoja na mwanafamilia mwingine mmoja wa nyumbani mwako.

Kwa sasa, kifurushi cha watu wawili kinapatikana tu katika nchi zifuatazo:

  • Australia
  • Ufaransa
  • Hong Kong
  • India (kinapatikana kwa watumiaji wachache)
  • Taiwani

Jinsi Kifurushi cha watu wawili kinavyofanya kazi:

Vifurushi vya YouTube vya watu wawili hukuwezesha kutumia manufaa yako ya uanachama pamoja na mwanafamilia mwingine mnayeishi katika nyumba moja.

  • Msimamizi wa familia:
    • Ndiye mmiliki wa akaunti ya msingi
    • Hulipia uanachama
    • Huanzisha kikundi cha Familia kwenye Google na hudhibiti kuweka na kuwaondoa wanafamilia
  • Mwanafamilia unayetumia naye:
    • Hutumia akaunti yake ya Google kufikia uanachama unaotumiwa pamoja
    • Ana mapendekezo, usajili na maktaba yake binafsi–hatutaruhusu ufikiaji wa mapendeleo ya kutazama au historia ya video zilizotazamwa kwenye akaunti za wanafamilia
    • Mipaka ya umri inatumika kwa wanafamilia walio na umri wa chini ya miaka 18

Kuanzisha Kifurushi cha watu wawili

Ili uanzishe Kifurushi cha watu wawili kwenye YouTube Premium:

  1. Nenda hapa ili uchague uanachama wa Kifurushi cha watu wawili.
  2. Chagua Kifurushi cha watu wawili.
  3. Ingia ukitumia akaunti yako ya Google.
  4. Thibitisha maelezo ya kulipa.
  5. Chagua Jisajili.
  6. Weka au uwaondoe wanafamilia kwenye kifurushi chako.

Ili uanzishe Kifurushi cha watu wawili kwenye YouTube Music Premium:

  1. Nenda hapa ili uchague uanachama wa Kifurushi cha watu wawili.
  2. Chagua Kifurushi cha watu wawili.
  3. Ingia ukitumia akaunti yako ya Google.
  4. Thibitisha maelezo ya kulipa.
  5. Chagua Jisajili.
  6. Weka au uwaondoe wanafamilia kwenye kifurushi chako.

Kudhibiti Kifurushi cha watu wawili

Iwapo wewe ni Msimamizi wa familia, unaweza kumwalika mtu mwingine mmoja kwenye Kifurushi chako cha watu wawili. Mtu huyo uliyemwallika anapaswa kuishi katika nyumba moja na Msimamizi wa familia yako.

Ili umwongeze mwanafamilia kwenye Kifurushi chako cha watu wawili:

  1. Ingia katika Akaunti ya Google inayohusishwa na uanachama wako unaolipiwa kwenye YouTube.
  2. Katika programu ya YouTube , gusa picha yako ya wasifu kisha Mipangilio .
  3. Chagua Ununuzi na uanachama.
  4. Gusa uanachama wako.
  5. Gusa Badilisha karibu na mipangilio ya Kutumia pamoja na familia.
  6. Gusa Alika mshirika.
  7. Weka anwani ya barua pepe ya mtu ambaye ungependa kumwalika.
  8. Chagua Tuma. Utapokea arifa ya barua pepe mtu anapojiunga na kifurushi chako.

Ili umwondoe mwanafamilia kwenye Kifurushi chako cha watu wawili:

  1. Ingia katika Akaunti ya Google inayohusishwa na uanachama wako unaolipiwa kwenye YouTube.
  2. Katika programu ya YouTube , gusa picha yako ya wasifu kisha Mipangilio .
  3. Chagua Ununuzi na uanachama.
  4. Gusa uanachama wako.
  5. Gusa Badilisha karibu na mipangilio yako ya Kutumia pamoja na familia.
  6. Chagua jina la mtu ambaye ungependa kumwondoa.
  7. Bofya Thibitisha.

Kukatisha Kifurushi cha familia na kuanzisha ya Kifurushi cha Watu wawili

Kumbuka: Ikiwa tayari unadhibiti uanachama wa Kifurushi cha familia cha YouTube Premium au cha YouTube Music Premium, utahitaji kukatisha uanachama wako kabla ya kujisajili kwenye Kifurushi cha watu wawili. Jisajili tena mwishoni mwa kipindi chako cha sasa cha kutozwa ili uepuke kutozwa mara mbili.

Ili ukatishe Mpango uliopo wa familia:

  1. Gusa picha yako ya wasifu kisha Ununuzi na uanachama.
  2. Gusa Mpango wa familia.
  3. Gusa Endelea ili ukatishe.
  4. Chagua sababu ya kukatisha kisha uguse Endelea.
  5. Gusa Ndiyo, katisha.

Ili ujisajili tena kwenye Kifurushi cha watu wawili:

  1. Kwenye programu ya YouTube , gusa picha yako ya wasifu.
  2. Chagua Pata YouTube Premium.
  3. Chagua Kifurushi cha watu wawili.
  4. Ingia katika akaunti yako ya Google.
  5. Utapata uthibitisho wa ununuzi, chagua Sawa.

Ukishajisajili kwenye Kifurushi cha watu wawili, utahitaji kuchagua mwanafamilia wako mpya kutoka katika Familia yako iliyopo.

Ili uchague mwanafamilia wa ziada ambaye ni mwanafamilia aliyepo katika Familia yako kwenye Google:

  1. Ingia katika Akaunti ya Google inayohusishwa na uanachama wako unaolipiwa kwenye YouTube.
  2. Katika programu ya YouTube , gusa picha yako ya wasifu au mipangilio kisha Ununuzi na uanachama.
  3. Gusa uanachama wako.
  4. Gusa Badilisha karibu na mipangilio ya Kutumia pamoja na familia.
  5. Gusa Chagua mshirika.
  6. Chagua au uandike jina la mtu ambaye ungependa kumwalika.
  7. Mtu utakayemchagua atapokea mwaliko wa kukubali ombi lako.

Ili umwalike mwanafamilia wa ziada ambaye ni mwanafamilia mpya katika Familia yako kwenye Google:

  1. Ingia katika Akaunti ya Google inayohusishwa na uanachama wako unaolipiwa kwenye YouTube.
  2. Katika programu ya YouTube , gusa picha yako ya wasifu au mipangilio kisha Ununuzi na uanachama.
  3. Gusa uanachama wako.
  4. Gusa Badilisha karibu na mipangilio ya Kutumia pamoja na familia.
  5. Gusa Alika mshirika.
  6. Gusa Thibitisha ili uwe msimamizi wa familia.
  7. Andika jina la mtu ambaye ungependa kumwalika.
  8. Mtu utakayemchagua atapokea mwaliko wa kukubali ombi lako.
Kumbuka: Msimamizi wa familia pekee ndiye anaweza kuchagua na kubadilisha mwanafamilia wa ziada.

Masharti ya Kifurushi cha Watu Wawili

Masharti ya msimamizi wa familia

Ukiwa Msimamizi wa familia, una wajibu wa kufanya uamuzi kuhusu uanachama kwa niaba ya Kikundi cha familia katika Kifurushi cha watu wawili. Utaweka maelezo ya mahali walipo wanafamilia na utaweza kumwalika mwanafamilia wa ziada kwenye Kifurushi chako cha watu wawili.

Ili utumie Kifurushi chako cha YouTube cha watu wawili pamoja na Kikundi chako cha familia, ni lazima:

  • Uwe na umri wa miaka 18 au zaidi (au umri unaofaa katika eneo uliko).
  • Uwe na Akaunti ya Google. Iwapo una akaunti ya Google Workspace, utahitaji kufungua au kuingia katika akaunti ya kawaida ya Google.
  • Uwe unaishi katika nchi au eneo ambako Vifurushi vya watu wawili vya YouTube Premium au YouTube Music vinapatikana kwa sasa: India, Ufaransa, Taiwani, Hong Kong na Australia.
  • Usiwe katika Kikundi kingine cha familia.
  • Uwe hujabadilisha Vikundi vya familia katika miezi 12 iliyopita.

Masharti ya wanafamilia

Ili ujiunge na Kikundi cha familia kinachotumia pamoja Kifurushi cha watu wawili cha YouTube Premium au cha YouTube Music Premium, ni lazima:

  • Uwe na akaunti ya Google. Iwapo una akaunti ya Google Workspace, utahitaji kufungua au kuingia katika akaunti ya kawaida ya Google.
  • Uwe unaishi katika nyumba moja na Msimamizi wa familia yako.
  • Uwe unaishi katika nchi au eneo ambako Vifurushi vya watu wawili vya YouTube Premium au YouTube Music Premium vinapatikana: India, Ufaransa, Taiwani, Hong Kong na Australia.
  • Usiwe katika Kikundi kingine cha familia.
  • Uwe hujabadilisha Vikundi vya familia katika miezi 12 iliyopita.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
14450133858099115395
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
false
true
true
true
true
true
59
false
false
false
false