Unaweza kuchagua au kubadilisha mipangilio yako ya manukuu kwenye TV, kifaa cha michezo ya video au kifaa chochote cha kuhifadhia data kinachotumia YouTube.
- Simamisha video unayocheza.
- Gusa Manukuu
.
- Chagua lugha ambayo ungependa kuangalia manukuu.
- Chagua muundo wa Manukuu.
- Chagua mipangilio ambayo ungependa kuiwekea mapendeleo. Unaweza kubadilisha fonti na mwonekano wake. Unaweza pia kubadilisha mandharinyuma na dirisha linalotumika kuonyesha manukuu.
Kumbuka:
- Ikiwa video haina manukuu,
inaweza kuonekana lakini haitaweza kuchaguliwa. Ikiwa
haionekani, manukuu hayapatikani katika video hiyo.
- Ikiwa video haina manukuu, inamaanisha kuwa mmiliki hakuweka manukuu au YouTube haikuweka manukuu kiotomatiki.